Serikali imepongezwa kwa kuandaa Jukwaa la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini (LCCF 2026), ambalo limeelezwa kuwa limekuwa na manufaa makubwa kwa wadau wa sekta hiyo, hususan wachimbaji wadogo.

Kupitia jukwaa hilo, washiriki wamepata elimu na maarifa ya kuwasaidia kuboresha shughuli zao, sambamba na kubadilishana uzoefu na wadau mbalimbali wa sekta ya madini kutoka ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Washiriki wameeleza kuwa majukwaa ya aina hii yanaendelea kufungua fursa za ushirikiano, kujifunza teknolojia na mbinu bora za uchimbaji, hatua inayotarajiwa kuongeza tija na kuimarisha ushiriki wa Watanzania katika sekta ya madini.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *