
Ripoti nchini Marekani zinaonyesha kuwa Rais wa
Marekani Donald Trump ameamuakutochukua hatua itakayoongeza ukubwa wa shambulio
la kijeshi la Marekani dhidi ya Iran, huku usiku mwingine ukipita bila
mashambulio ya anga katika eneo hilo.
Ripoti zinaonyesha kuwa maafisa wa Marekani
wameelezea wasiwasi wao kuhusu kupungua kwa akiba ya makombora ya Patriot,
pamoja na uwezekano wa kuwatenga washirika wa Kiarabu katika eneo la
Ghuba—jambo ambalo linaweza kufufua matumaini ya kurejea kwenye mazungumzo
baada ya karibu wiki mbili za msururu wa mashambulizi ya anga ya Marekani.
Tangu jioni ya Ijumaa, Marekani haijafanya
mashambulizi ya anga dhidi ya Iran, bila kutoa maelezo yoyote rasmi kuhusu
uamuzi huo; hata hivyo, ripoti mbalimbali za vyombo vya habari zilisema kuwa
Trump aliamua siku ya Ijumaa kusitisha mashambulizi hayo ya anga.
Axios iliripoti kuwa Pentagon iliwasilisha kwa
Trump mpango wa kufanya mashambulizi ya anga, lakini alikataa kuuidhinisha,
akipendelea zaidi kutafuta suluhu kupitia mazungumzo.
Kauli pekee rasmi kuhusu suala hilo ilitoka kwa
msemaji wa Ikulu ya Marekani, ambaye alisema kuwa Trump siku zote hupendelea
suluhu ya kidiplomasia.
Huku hayo yakijiri Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Ismail Baghaei, alisema kuwa hakuna kilichobadilika kuhusu usafiri wa meli kwenye Lango la Hormuz.
Akijibu swali la waandishi wa habari kuhusu mazungumzo kati ya Iran na Oman kuhusu Lango la Hormuz, Baqaei alieleza kuwa duru kadhaa za mazungumzo kati ya Iran na Oman zilifanyika siku ya Ijumaa na Jumamosi.
Katika mazungumzo hayo, pande hizo mbili zilijadili kanuni za pamoja na taratibu za kiutendaji za kusimamia usafiri salama wa majini katika Lango la Hormuz, huku zikiheshimu mamlaka ya nchi hizo mbili zenye mwambao wa pwani.
Ujumbe wa Oman uliondoka Tehran Jumamosi jioni, kulingana na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, ambaye alisema kuwa mazungumzo hayo yamepiga hatua na kuleta matokeo chanya, huku akiongeza kuwa mashauriano ya kiufundi na kisiasa kati ya pande hizo mbili bado yanaendelea.
Maelezo zaidi: