Dar es Salaam. Katika makazi yake Sinza ile ya Vatcan. Kwenye uchochoro yalipo makazi yake. Halikuwa eneo bora na rafiki kwa maegesho ya magari. Ni makazi ambayo haya-kuendana na uzito wa kazi na jina lake. Ni nani huyo? Wewe nata na biti la maandi-shi haya.

Aliipenda Sinza kwa makazi na kiofisi. Aliishi Vatcan ofisi ikiwa Mori. Kama una-vyojua Sinza ni eneo la mishe mishe nyingi kwa Dar. Watu kibao huona utamu wa maisha ya Sinza kwa ‘bizinesi’, bata na kupata huduma yoyote utakayo na muda wowote.

Kinachofanya Sinza ivutie ni laifu la usiku. Baa, lounge, ‘laivu bendi’ na viota vya ‘kumiti’ na masela. Misosi kama kiepe yai, mishikaki, nyama choma na migahawa ya kijanja. Dili za kukesha, maduka, saluni, pisi kali huko ndo kwenye zinapatikana kirahisi mchana na usiku.

Usafiri wa uhakika. Ni rahisi kupata boda, bajaji na usafiri wa mtandaoni. Mchang-anyiko wa watu, madenti wa vyuo wengi wamepanga Sinzani. Kubwa ni wasanii wengi wanaishi Sinzani, na kufanya kiwe kitongoji chenye mzuka. Miaka na miaka Sinza ni kitaa cha mastaa.

Kama maeneo ya Kariakoo yenye mishe nyingi. Sinza pia hupatwa na foleni, kelele na gharama za maisha ambazo zinaweza kuwa juu kulinganisha na baadhi ya mae-neo mengine. Watu wengi husema raha ya Sinza unapata chochote na muda wowote na kwa yeyote.

Ikulu ya Magogoni ikahamia pale Vatcan. Na JK alitimba eneo hilo. `Of coz` Waziri Mkuu wa wakati ule Mh. Pinda alitimba. JK afike wewe nani asifike? Mastaa wote walifika. Watu walilia kuliko kilio walicholia ndugu zao waliofariki. Walimpenda naye alijipenda na

Kazi yake ilipendwa.

Taarifa ya kifo chake ilisambaa usiku mnene hadi jua linaanza kuchomoza kwenye mawimbi ya bahari ya Hindi. Tayari Sinzani ilikumbwa na mafuriko ya watu wa kila aina. Hakuna aliyeamini. Kuanzia Shekilango mpaka kule Bamaga. Mitaa ilisizi ki-noma.

Picha za kipande cha mtu akiwa kafumba macho pale mochwari ya Muhimbili. Zilis-ambaa kwa kasi mitandaoni. Vilio vikasikika. Neno R.I.P Kanumba, likawa ni neno maarufu ghafla baada ya taarifa za kifo chake. Hakuugua wala afya yake haikuwa dhaifu umauti wa ghafla.

Ukiondoa kifo cha Baba wa Taifa. Ujio wa Papa John Paul wa Pili. Kuwasili kwa Man-dela. Hakuna tukio lililokusanya watu kama mazishi ya Kanumba. Leaders Club na Kinondoni Makaburini kulifurika. Watu walikanyagana huku mashavu yakimeremeta kwa machozi.

Umati ule uliwatia akili viongozi wengi. Hata wa kauli za “Who’s Diamond?” Ilijifia. Mazishi yale yalifanya wafute kauli zao. Ule ukubwa wa mazishi uliifanya wengi washituke na kugundua sanaa ni mtaji. Wasanii wakajua uzito wao na mapenzi ya watu kwao.

Mitazamo ya watu juu ya wasanii ikabadilika kabisa. Heshima ya ikapaa juu kama ndege joni. Kifo chake ni kama kilikuja kuwaokoa wana wa Israeli ya sanaa. Sanaa ikapaa juu kiheshima, ikaanza kiyumba sana kiubora. Mussa wa sanaa aliondoka na sanaa yake?

Shabiki wa Ferouz na shabiki wa Marioo wana mitazamo tofauti. Yule wa Ferouz aliamini sanaa ni umaarufu. Wa Marioo anaamini sanaa ni utajiri chekwa. Kati yao mmoja anaitazama sanaa kama shamba. Mwingine anaitazama sanaa kama njia.

Shabiki wa Ferouz aliamini ile ndinga alipewa na Rais Mkapa. Wakati huyu wa Mari-oo anaamini muziki unampa kila kitu katika hii dunia. Walio wengi hawakujua nguvu ya sanaa na wasanii wa Bongo. Vikauli kama “Supa staa Bongo bana?” Na dharau kwa wasanii zilitawala.

Leo hii Mondi ana rundo la ‘stafu’ kwa biashara zake. Kwa sababu ya sanaa yake tu. Miaka kadhaa iliyopita wasanii walishandana kwa kupanga nyumba Sinzani na mae-neo mengine. Leo wasanii wanashindana kununua viwanja na kujenga huko Goba, Madale nk.

‘Hu izi Diamond?” “Ustaa Bongo?” “Msanii Bongo?” Hivi ni vikauli vya kijinga vya wajinga wengi wa kitambo hicho. Sanaa ni kiwanda cha kutengeneza mastaa wenye utajiri. Zamani kilikuwa kiwanda cha kutengeneza mastaa wenye njaa. Mambo yamepinduka ‘nau deizi’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *