
Iran imetangaza kusitisha mashambulizi dhidi ya washirika wa Marekani kwenye eneo la mashariki ya Kati, tangazo lake likijiri baada Washington kusitishe mashambulizi dhidi ya Tehran.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Iran, Mohammad Akraminia, mashambulizi yao yanakoma mara moja kufuatia hatua ya Washington kusitisha mashambulizi yake siku mbili zilizopita.
Akraminia amesema, kwakuwa mashambulizi yao yalikuwa ni kujibu kinachofanywa na Marekani, na wao wameamua kusitisha operesheni zao dhidi ya nchi za ukanda.
Usitishwaji huu wa mapigano, umeibua matumaini mapya ya kurejelewa kwa mazungumzo baada ya karibu wiki mbili za mashambulio ya usiku na mchana yaliyofanywa na Marekani, hata hivyo wadadisi wa mambo wakisema huenda hatua hiyo inatokana na upungufu wa mitambo ya kudungua roketi za Iran.
Aidha Iran kwenye taarifa yake imedai kuwa itarejelea mashambulizi yake ikiwa Marekani itaamua kuishambulia tena, kauli inayotolewa wakati huu Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, akielekea washinhgton kwa mazungumzo na Rais Donald Trump, mshirika wake mkubwa kwenye vita ya Iran