Chama cha upinzani nchini Tanzania, Chadema, kimeendelea kuituhumu serikali kwa kutumia mashtaka ya ugaidi kama njia ya kuwanyamazisha wakosoaji wake licha ya utawala kukanusha madai hayo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake mwishoni mwa juma lililopita, makamu mwenyekiti wa Chadema, John Heche, alitolea mfano mashtaka mapya ya ugaidi waliyopewa wanachama wao zaidi ya 50 pamoja na mhadhiri mmoja wa chuo kikuu, akisema lengo ni kuwatisha wapinzani.

“Kesi za wale viongozi ni kesi zetu sote kama wanachadema tulioko nje.Katikia kipindi hiki, wanachadema tutapimwa na tutaona ni kwa kiasi kipi tunaamini yale tunayoyapigania.” Alisema John Heche.

Mashtaka haya yamefunguliwa wakati huu Tanzania ikikosolewa na watetezi za haki za binadamu wa ndani nan je Pamoja na baadhi ya Washirik awa kimataifa, Rais Samia Suluhu Hassan, akitetea namna Idara za usalama zinavyokabiliana na watu Pamoja na wanaharakati aliodai wanajihusisha na vitend vya ugaidi.

‘‘Sisi ni wafuasi wazuri sana wa haki za binadamu sasa haya yanayosemwa na mengine yatakayoendelea kusemwa sisi tunajielewa.’’ Alisema Rais Samia.

Samia Hassan- Rais wa Tanzania
Samia Hassan- Rais wa Tanzania REUTERS – Emmanuel Herman

Katika hatua nyingine, hapo jana jeshi la Polisi nchini humo, kupitia kwa msemaji wake David Misime, limesema watu 36 kati ya 130 waliokamatwa kwa tuhuma mbalimbali za uhalifu wamefikishwa mahakamani.

‘‘Wengine waliokuwa wakipanga na kuhamasisha mbali na kufanya fujo kupitia maandamano yasiofuata sheria, vitendo kama hivi vinaonyesha uwepo wa tuhuma za makosa ya kigaidi.’’ David Misime

Haya yanajiri wakati huu kinara wa upinzani na mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, akiwa kizuizini kwa zaidi ya mwaka mmoja kwa tuhuma za makosa ya ugaidi, kesi ambayo mwenyewe amesema imechochewa kisiasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *