Kinyang’anyiro cha kumsaka katibu mkuu ajaye wa Umoja wa Mataifa, sasa kimechukua sura mpya baada ya mgombea wa saba kujitokeza mwanadiplomasia wa Uganda, Olara Otunnu, ambaye ameteuliwa na serikali yake kuwania kiti hicho.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Otunnu, aliyewahi pia kuwa mgombea urais nchini humo, aliwahi pia kushika wadhifa wa juu kwenye umoja wa Mataifa, ikiwemo mjumbe maalumu wa katibu mkuu anayehusika na masuala ya watoto, wakati wa utawala wa Koffi Annan.

Otunnu pia aliwahi kuwa mgombea wa upinzani katika uchaguzi wa mwaka 2011, ambapo alishindwa vibaya na rais Yoweri Museveni, ambaye yuko madarakani tangu mwaka 1986.

Wagombea wengine wanaowania nafasi hiyo ni mkurugenzi wa shirika la nguvu za Atomiki, Rafael Grossi raia wa Argentina na zamani wa Chile Michelle Bachelet.

Wengine ni Makamu wa Rais wa zamani wa Costa Rica Rebeca Grynspan, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Ecuador Maria Fernanda Espinosa, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Guyana Carolyn Rodrigues-Birkett pamoja na Rais wa zamani wa Senegal Macky Sall.

Ili mgombea mmoja kupatikana, atalazimika kupata kura 9 bila kupigiwa kura ya turufu toka kwa nchi 5 wanachama wakudumu wa baraza la usalama, ambazo ni Marekani, Ufaransa, Uingereza, China na Urusi.

Baada ya hapo jina lake litatumwa katika kikao cha baraza la umoja wa Mataifa kuthibitishwa na atachukua rasmi madaraka Januari Mosi mwakani ambapo katibu mkuu wa sasa Antonio Guterrers atakuwa amemaliza muda wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *