Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Ismaeil Baqaei amelaani vikali shambulio la utawala wa Israel dhidi ya msafara wa kimataifa wa meli nyingi wa Sumud uliokuwa ukielekea Ukanda wa Gaza.

Msafara huo wa meli umeshambuliwa na jeshi la Israel katika maji ya kimataifa ambapo Israel imewatia nguvuni wanaharakati wanaowaunga mkono wananchi wa Palestina waliokuwa katika meli hizo. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametayataja mashambulizi ya Israel dhidi ya msafara wa Sumudkuwa ni kitendo cha kigaidi chenye lengo kuendeleza baa la njaa katika Ukanda wa Gaza.

Esmail Baqaei ameashiria kushiriki nchi 47 duniani katika kampeni ya kibinadamu ya Sumud iliyoratibiwa ili kuvunja mzingiro wa kidhalimu dhidi ya Gaza na kukabiliana na mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na Israel dhidi ya Wapalestina kusisitiza kuwa upo ulazima serikali zote na Umoja wa Mataifa kuunga mkono kampeni hii, kuuwajibisha utawala wa Kizayuni na kuwaachia huru haraka iwezekanavyo wanaharakati wote waliokuwa kwenye msafara huo. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran pia amegusia kushikiliwa wanaharakati wa msafara wa Sumud katika jela ya Katziyot inayojulikana kwa sifa mbaya ya mateso na ukatili wa utawala ghasibu dhidi ya wafungwa wa Kipalestina na kusema: “Kutiwa mbaroni wanaharakati wanaoiunga mkono Palestina na kuhamishiwa katika jela hiyo pamoja na tabia ya udhalilishaji ya Waziri wa Usalama wa Ndani wa Israel dhidi yao, ni ishara nyingine ya kuporomoka kwa maadili utawala wa Kizayuni. 

Baqaei pia amebainisha kuchukizwa kwake na himaya na uungaji mkono endelevu wa Marekani na baadhi ya nchi za Magharibi kwa mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya Wapalestina na kusema serikali zote zina wajibu wa kisheria na kimaadili kukomesha mauaji hayo ya kimbari na kuchukua hatua ya kuwaadhibu wahalifu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *