#HABARI: Bodi ya Korosho Tanzania(CBT) imetoa tuzo ya Muandishi Bora wa Taarifa za Korosho kundi la Runinga, kwa mwandishi wa ha…#HABARI: Bodi ya Korosho Tanzania(CBT) imetoa tuzo ya Muandishi Bora wa Taarifa za Korosho kundi la Runinga, kwa mwandishi wa ha…

#HABARI: Bodi ya Korosho Tanzania(CBT) imetoa tuzo ya Muandishi Bora wa Taarifa za Korosho kundi la Runinga, kwa mwandishi wa habari wa ITV/Radio One mkoa wa indi, Bi. Fatuma Maumba.

Tuzo hiyo imekabidhiwa na Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe, katika Mkutano Mkuu wa Wadau wa Tasnia ya Korosho nchini, uliofanyika Jijini odoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania(CBT), Bw. Francis Alfred amepongeza mchango mkubwa unaotolewa na vyombo vya habari vya habari kupitia kwa waandishi wao.

Kwa upande wa Runinga, walioshindanishwa tuzo hiyo ni pamoja na Fatuma Maumba wa ITV mkoa wa Lindi, Mariamu Maregesi ZBC mkoa wa Mtwara na Emmanuel Msigwa wa ITV mkoa wa Ruvuma na kupelekea mshindi wa tuzo hiyo kuwa Fatuma Maumba.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *