Umoja wa Ulaya umetangaza siku ya Jumatano, Oktoba 22, kwamba umefikia makubaliano ya kuimarisha vikwazo vyake dhidi ya hidrokaboni za Urusi na kuzuia rasilimali za Kremlin katika vita vyake dhidi ya Ukraine. Marekani imefuata mkondo huo haraka, na kuamua juu ya vikwazo dhidi ya kampuni za mafuta za Urusi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Matangazo haya yanakuja baada ya usiku mwingine wa mashambulizi ya Urusi kote Ukraine, na zaidi ya drone 400 na baadhi ya makombora thelathini kurushwa. Mashambulizi haya yamesababisha vifo vya watu wasiopungua sita. Duru ya 19 ya vikwazo vya Umoja wa Ulaya, ambapo Denmark ambayo ni mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya (EU) imetangaza makubaliano Jumatano jioni, ni pamoja na kusitisha kabisa uagizaji wa gesi ya kimiminika ya Urusi (LNG) na hatua za ziada dhidi ya kundi la meli za mafuta zinazotumiwa na Moscow kukwepa vikwazo vya Magharibi.

“Upitishaji rasmi wa nakala umepangwa kesho (Alhamisi, Oktoba 23). “Washington imetangaza mara moja kwamba inapanga kuimarisha vikwazo vyake dhidi ya Moscow. Haya yamethibitishwa rasmi mara moja.

“Tutatangaza, leo baada ya kufungwa (kwa Wall Street) au mapema kesho asubuhi, kuimarishwa kwa vikwazo dhidi ya Urusi,” Waziri wa Fedha wa Marekani Scott Bessent amewaambia waandishi wa habari katika Ikulu ya White House siku ya Jumatano. Mwishowe, tangazo limekuja haraka sana.

Wizara ya Fedha ya Marekani imetangaza vikwazo vinavyolenga makampuni ya mafuta ya Urusi Rosneft na Lukoil. Hii, kulingana na Washington, ni athari ya “Urusi kutokuwa na nia ya dhati ya kushiriki katika mchakato wa amani kumaliza vita nchini Ukraine.”

Kulingana na Trump, mazungumzo na Putin “hayafiki popote”

“Kutokana na kukataa kwa Rais Putin kusitisha vita hivi visivyo na maana, Wizara ya fedha inaweka vikwazo kwa makampuni mawili makubwa ya mafuta ambayo yanafadhili vita ya Kremlin,” amesema Scott Bessent.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *