DURBAN – Viongozi katika sekta ya afya , wanasayansi na wataalam wanakutana jijini Durban nchini Afrika Kusini ,kujadili mpango wa pamoja wa kufadhili sekta ya afya baada ya miradi nyingi barani kuathirika na kupunguzwa kwa ufadhili wa kigeni haswa na nchi ya Marekani.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kongamano hili, linalofanyika kuelekea kongamano la G20 linalenga kuja na sauti ya pamoja ya Afrika ya kuwa na usalama katika sekta wa afya.
Daktari Jean Kaseya ni mkurugenzi wa kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa, Afrika CDC,ni mwenyeji wa kikao hicho.
“Mpango wa kwanza mbadala, ni ufadhili wa ndani ya nchi tofauti ,nchi ziwekeze zaidi kwenye sekta ya afya”

Profesa Omu Anzele kutoka chuo kikuu cha Nairobi nchini Kenya anasema, mataifa ya Afrika yanapaswa kuanza kufikiria namna ya kutafuta ufadhili nje ya mataifa ya Magharibi, kama Marekani.
“Tuangalie wadau wapya wanaoweza kutusaidia kama wale kutoka bara Asia” Amesema.
Shiva Murugasampilay kutoka taasisi ya afya ya umma Zimbabwe anapendekeza waafrika kukumbatia mbinu za kuzuia magonjwa, badala ya kuyatibu.
“Sharti tubadilishe mifumo yetu, kutoka hospitalini,kutibu magonjwa hadi kuzuia magonjwa kwa kuishi maisha yenye afya”
Vitengo vya afya ambavyo vimeathirika na kupungua ufadhili wa kigeni barani Afrika ni pamoja na Malaria,Virusi vya Ukimwi, Kifua Kikuu na utoaji chanjo.