#HABARI:Chama cha Demokrasia na mandeleo CHADEMA kimesema kuwa Makamu Mwenyekiti Taifa Mh.John Heche anashikiliwa kwenye mahabusu ya Jeshi la Polisi Mtumba , jijini Dodoma.
Taarifa hiyo ya CHADEMA inasema kuwa Heche alifanyiwa mahojiano na Idara ya Uhamiaji mbele ya wakili wa Chama na Kaka yake jana Ijumaa Oktoba 25,2025 kwa tuhuma za kuvunja Sheria za Uhamiaji kwa kile kilichotajwa cha kuvuka mpaka wa Tanzania na kuingia nchini Kenya bila kufuata utaratibu.
Taarifa hiyo pia imebainisha kuwa Heche amekosa dhamana licha ya kosa hilo kuruhusu mtuhumiwa kupewa dhamana.
Ikumbukwe kuwa kiongozi huyo wa CHADEMA John Heche alikamatwa na Jeshi la Polisi siku ya Jumatano kwenye geti la Mahakama Kuu Masjala ya Dar es Salaam.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania