RSF hivi karibuni imechukua sehemu kubwa eneo la El Fasher katika jimbo la Darfur Kaskazini na jiji la Bara katika jimbo la Kordofan Kaskazini, jambo ambalo limeongeza hofu ya mateso makubwa kwa raia.
Raia wanaadhibiwa El Fasher
“Katika eneo la El Fasher, taarifa za awali zinaonesha hali hatarishi sana tangu RSF ilipotangaza wameshika udhibiti wa kikosi cha 6 cha askari wa miguu,” amesema Kamishina Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk. “Hali ya kuongezeka kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unaochochewa na ubaguzi wa kikabila katika mji wa El Fasher inazidi kuongezeka kila siku. Hatua za dharura zinahitajika ili kulinda raia.”
Ameongeza kuwa ” Video za kusikitisha zinaonesha wanaume wengi wasio na silaha wakiuawa au wakiwa wamezama kwenye maiti, wakidaiwa kuwa wanajeshi wa Jeshi la Sudan”.
Watu waliofurushwa makwao Sudan watafuta hifadhi Tawila.
Kufungwa Kwa miji kumeongeza mgogoro wa kibinadamu
Kati ya mzingizro wa miezi 18 wa RSF, raia wanakumbwa na uhaba mkubwa wa chakula na gharama za juu. Türk amebainisha kuhusu ripoti za wanaume watano kuuawa kwa kujaribu kupeleka chakula El Fasher.
Amesema Mamia wengine, wakiwemo wanahabari, wamedhibitiwa wanapojaribu kutoroka. Umoja wa Mataifa pia umeonya kuwa uwezekano wa unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana ni mkubwa kutokana na mifumo iliyopita katika jimbo la Darfur Kaskazini.
Ukatili unasambaa Kordofan Kaskazini
Mauaji ya kikatili pia yameripotiwa katika jiji la Bara, Kordofan Kaskazini, kufuatia kushikiliwa kwake na RSF tarehe 25 Oktoba.
Waathirika walidaiwa kuwa wanasiasa au wafuasi wa Jeshi la Sudan. “RSF lazima ichukue hatua za dharura kumaliza na kuzuia ukatili dhidi ya raia katika mji wa El Fasher na Bara,” amesema Türk, akisisitiza kuwa sheria za kibinadamu za kimataifa zinakataza ukatili dhidi ya wale wasiokuwa sehemu ya mapigano.
Wito kwa jamii ya kimataifa
Türk amezitaka nchi wanachama zenye ushawishi kwa RSF kuchukua hatua mara moja ili kuzuia utekaji wa mateso zaidi.
Amesema “Kuhakikisha uwajibikaji kwa ukiukaji wa sheria za kibinadamu na haki za binadamu na pande zote za mzozo ni muhimu kuzuia mzunguko mpya wa ukiukaji wa haki za binadamu.”
Amemalizia kwa kusema kwamba Umoja wa Mataifa unaendelea kufuatilia hali hii, akisisitiza umuhimu wa kufikisha msaada wa kibinadamu na kulinda raia.