Mradi wa We-Fi unalenga kufungua uwezo wa wajasiriamali wanawake kwa kuwapatia mitaji, misaada ya kiufundi, na huduma shirikishi, mradi huu ukiwa ni ushirikiano wa serikali ya Tanzania, Benki za Kimataifa za Maendeleo na wadau wengine. Hoteli ya Mbezi Garden ni miongoni mwa biashara zilizotwamishwa na coronavirus“>COVID-19, mmiliki wake Bi. Lawere mnufaika wa mradi wa We-Fi anasema, fedha nilizochukua niliweza kuwekeza tena kwenye biashara. Kwa hiyo wakati najikwamua kutoka kwenye COVID-19 nilishakuwa nimejenga mgahawa, kumbi, vyumba vya malazi. Kwa hiyo biashara ziliporejea katika hali ya kawaida nilikuwa tayari nimejiandaa kupokea tena wageni, na hii ilikuwa hatua nzuri sana wakati huo.”

Kuimarika kwa mjasiriamali Haika, kumeleta manufaa kwa wafanyakazi wa hoteli anayomiliki inayotoa huduma za kumbi za sherehe, vyakula na vinywaji.

Shadrack Mwitura ni miongoni mwa wafanyakazi akiwa na nafasi ya Meneja akisimamia shughuli za kumbi ikiwemo semina na kupokea wageni. Alianza kazi kwenye kampuni hii mwaka 2005 akiwa mhudumu na kupanda cheo hadi kuwa Meneja.

Nilianza na kipato kidogo, lakini kadri nikipandishwa cheo, na mshahara nao unaongezeka. Nikipokea mshahara kwanza ninaugawa kwanza chakula, ada, usafiri na akiba ninaweka benki.”

Mjasiriamali wa kike Haika Lawere na wafanyakazi wenzake jijini Dar Es Salaam, Tanzania.

© World Bank

Mjasiriamali wa kike Haika Lawere na wafanyakazi wenzake jijini Dar Es Salaam, Tanzania.

Naye Mosi Mohammed, mhudumu ni mama wa watoto watatu. Anasema, “niliolewa lakini nimeachika, sasa ninalea watoto wangu peke yangu. Nilianza kama kibarua, lakini baadaye kazi yangu ikaonekana na hivi sasa ni mhudumu. Ninapenda kazi yangu kwa sababu ndio inaniwezesha kutunza familia yangu.”

Kwa Mosi, kuwa na ajira kunamfanya ajisikie vizuri. “Ninajisikia vizuri kuwa mwajiriwa, kwa sababu kuna vitu vingi, kando ya mshahara nitavipata hapo baadaye. Kwanza mimi niña watoto, kuna zile bima za afya. Sasa hivi ninakusanya fedha kwa ajili ya kuweka umeme kwenye nyumba yangu.”

Tangu kuanza kwa mradi huu wa We-Fi, mwaka 2017, zaidi ya wanawake 500,000 kutoka mataifa 83 wamenufaika kwa kupatiwa mitaji,  masoko na stadi bora za kuimarisha biashara zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *