Hayo yamesemwa bungeni na waziri mmoja, wakati taifa hilo likiimarisha vita vyake dhidi ya makundi ya ulaghai kufuatia hasara kubwa kabisa inayosababishwa na ulaghai. Waziri mwandamizi wa masuala ya ndani wa Singapore Sim Ann ameliambia bunge kuwa taifa hilo la pili kwa ukubwa kiuchumi Kusini-mashariki mwa Asia lilipoteza zaidi ya dola bilioni 2.8 kupitia ulaghai kuanzia mwaka wa 2020 hadi nusu ya kwanza ya 2025.

Amesema kumekuwa na visa 190,000 vya ulaghai vilivyoripotiwa katika kipindi hicho. Sasa amesema wataanzisha adhabu ya kuwachapa fimbo walaghai. Hii ni baada ya kuufanyia marekebisho mswada wa sheria ya uhalifu ya Singapore uliowasilishwa kwa mara ya pili bungeni.

Waziri Sim amesema “Wahalifu wanaofanya ulaghai, unaofafanuliwa kama kudanganya hasa kwa njia ya mawasiliano iwe ni simu au intaneti, wataadhibiwa kwa kuchapwa viboko sita.” Na wale wanaowasaidia matapeli, wakiwemo wanaoitwa “watu wanaouza pesa” ambao hutoa akaunti za benki au kadi za simu, wanaweza kupewa adhabu ya kupigwa hadi viboko 12, kulingana na muswada huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *