Chama Kikuu cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA, kimesema Makamu Mwenyekiti wake John Heche amefunguliwa mashtaka ya ugaidi, siku chache baada ya kukamatwa kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa Oktoba tarehe 29, uliokumbwa na machafauko yanayoripotiwa yalisababisha vifo vya mamia ya waandanamanaji.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kupitia ukurasa wake wa X, chama hicho kimesema, Heche ambaye alikamatwa jijini Dar es salaam, Oktoba 22, amefunguliwa mashtaka hayo, ambayo hayana dhamana nchini Tanzania.

Aidha, chama hicho kimesema kiongozi huyo amekataa kuadiksha taarifa, baada ya mahoajino na sasa anasubiri kufikishwa Mahakama, ambapo mpaka sasa haijafamika ni lini hilo litafanyika.

Haya yanajiri wakati huu Mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu, aliyekamatwa mwezi Aprili na kufunguliwa kesi ya uhaini, kesi yake ikiendelea jijini Dar es salaam.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu, kama Amnesty International na Human Rights Watch, yameendelea kulaani hatua ya serikali nchini Tanzania, kuendelea kuwahangaisha wanasiasa wa upinzani na kuminya haki zao za kujieleza

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *