Waangalizi wa uchaguzi kutoka Umoja wa Afrika katika ripoti yao ya baada ya uchaguzi wa Tanzania wanasema zoezi hilo halikuzingatia kanuni za kidemokrasia, uchaguzi ambao uligubikwa na vurugu siku ya upigaji kura.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Rais Samia Suluhu Hassan alitangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, uchaguzi ambao hata hivyo wapinzani wake wakuu waliozuiliwa kushiriki, walisema ulikumbwa na udaganyifu mkubwa.

Kulingana na waangalizi hao kutoka AU, uchaguzi wa mwaka huu nchini Tanzania ulikosa kabisa kuafikia vigezo vya AU kuhusu uchaguzi sawa na kanuni zengine za kimataifa za uchaguzi wa demokrasia.

Rais Samia Suluhu Hassan wakati akiapishwa jijini Dodoma, 03/11/25.
Rais Samia Suluhu Hassan wakati akiapishwa jijini Dodoma, 03/11/25. via REUTERS – PRESIDENTIAL PRESS UNIT

Aidha waangalizi hao wanasema walibaini kuwa baadhi ya masanduku ya kupiga kura tayari yalikuwa yamejazwa makaratasi ya kupiga kura kwenye vituo vya kupiga kura.

Vilevile AU inasema maejenti wa vyama vya kisiasa hakuwa kwenye vituo vya kupiga kura ambapo pia wakati wa zoezi la kuhesabu kura baadhi ya waangalizi walitakiwa kuondoka vituoni.

Kwa upande wake serikali ya Tanzania inasisitiza kwamba uchaguzi huo ulikuwa wa huru na haki.

Mazishi ya mtu aliyeuawa wakati wa maandamano ya uchaguzi nchini Tanzania
Mazishi ya mtu aliyeuawa wakati wa maandamano ya uchaguzi nchini Tanzania AP

Katika hatua nyengine, chama kikuu cha upinzani chadema licha ya kuzuiwa kushiriki kwenye uchaguzi huo, kimesisitiza kuwa kimerekodi vifo vya mamia ya watu waliouawa wakati wa maandamano ya uchaguzi wa Tanzania.

Naye Boniface Mwabukusi,Rais wa chama cha mawakili wa  Tanganyika ambacho kinawaleta pamoja mawakili kutoka Tanzania bara alisema kwamba wanakadiria kuwa zaidi ya watu Elfu 1 waliuawa kwenye maandamano hayo kwa mujibu wa takwimu za ndani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *