Johan Borgstam, Mjumbe maalum wa Umoja wa Ulaya kwa kanda ya Maziwa Makuu, ana wasiwasi kuhusu hali ya mashariki mwa DRC. Anahitimisha ziara ya siku nyingi nchini humo, ikiwa ni ziara yake ya saba katika kanda hiyo tangu ateuliwe katika wadhifa wake mnamo Septemba 2024.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ingawa Johan Borgstam, Mjumbe Maalum wa Umoja wa Ulaya, EU, kwa kanda ya Maziwa Makuu, anakaribisha majadiliano yanayoendelea huko Doha na Washington, anabainisha hali ya usalama mashariki mwa DRC bado inatia wasiwasi sana.

“Inanipa matumaini makubwa kufuata juhudi za Marekani na Qatar katika mchakato wa amani huko Doha. Umoja wa Ulaya unatoa msaada wake, hilo liko wazi. Kwa upande mwingine, ninaposafiri pia katika kanda hiyo, nimezungumza na wakimbizi wa Kongo.” “Kwangu mimi, ninachojifunza kutoka kwa hili ni kwamba kwa bahati mbaya kuna mgawanyiko mkubwa na mtengano kati ya hali halisi ya kidiplomasia kwa upande mmoja na hali halisi mashinani kwa upande mwingine. Kwangu mimi, hii pia inaangazia umuhimu wa Umoja wa Ulaya kuunga mkono kikamilifu michakato hii ili malengo ya mazungumzo yatimie,” ameeleza.

Kufungua upya Uwanja wa Ndege wa Goma

Johan Borgstam pia ana wasiwasi kuhusu hali ya kibinadamu. Umoja wa Ulaya unatoa wito wa kufunguliwa tena kwa Uwanja wa Ndege wa Goma, angalau kwa ndege za zinzosafirisha misaada ya kibinadamu. “Pande zote katika eneo hilo zina majukumu yaliyo wazi. Ni muhimu sana kwamba Uwanja wa Ndege wa Goma ufunguliwe tena, hata kwa kiwango kidogo. Kwa watu wanaoteseka Mashariki, kuweza kuwezesha safari chache za ndege za kibinadamu kunaonyesha watu walio eneo hilo kwamba kuna kitu kinachotokea. Hatupaswi kupuuza umuhimu wa safari za ndege, hata zile za mfano,” amehitimisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *