
Hata hivyo, mahakama hiyo yenye makao makuu yake mjini The Hague nchini Uholanzi, hairuhusu kusikilizwa kwa kesi bila uwepo wa mshitakiwa mahakamani.
Mara ya mwisho kwa Kony kuonekana hadharani ilikuwa ni mwaka 2006.
Kulingana na majaji wanaoshughulikia kesi hiyo, kuna kila msingi wa kuamini kuwa Kony alikuwa akihusika na makosa hayo 39.
Makosa hayo ni pamoja mashambulizi ya LRA dhidi ya shule na kambi za watu waliokosa makazi, utesaji wa watu, ndoa za kulazimisha, ubakaji na kadhalika.