Rais wa Marekani amebainidha siku ya Alhamisi kwamba mpango wa nyuklia wa Iran “umeangamizwa” na mashambulizi ya Marekani yaliyofanywa mwishoni mwa mwezi wa Juni.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Donald Trump amesema siku ya Alhamisi kwamba Iran iliomba kuondolewa kwa vikwazo vya Marekani na iakasema “yuko wazi” kwa majadiliano. “Iran imeomba vikwazo hivyo viondolewe,” rais wa Marekani amesema wakati wa chakula cha jioni na viongozi wa Asia ya Kati.

“Iran ina vikwazo vizito sana vya Marekani, na hilo linawafanya iwe vigumu sana kwao kufanya kile ambacho wangependa kuweza kufanya, na mimi niko wazi kusikia hilo. Tutaona kitakachotokea, lakini mimi niko wazi kwa hilo,” ametangaza.

“Iran ilikuwa mnyanyasaji wa Mashariki ya Kati … ambayo kwa sasa imesitisha vitendo vyake viovu,” Donald Trump ameongeza, akidai kwamba mpango wa nyuklia wa Iran “umeangamizwa” na mashambulizi ya Marekani yaliyofanywa mwishoni mwa mwezi Juni.

Iran na vikwazo vingi

Marekani imeweka vikwazo vingi vya kiuchumi na kijeshi dhidi ya Iran tangu Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979, ikiwa ni pamoja na vikwazo vinavyokataza biashara yote na Tehran.

Rais wa Marekani ametangaza mfululizo wa hatua dhidi ya Tehran tangu kurejea madarakani mwezi Januari. Wakati wa muhula wake wa kwanza, alijiondoa kwenye makubaliano ya kimataifa ya 2015 kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran (JCPOA), ambayo yalijumuisha kuondolewa kwa vikwazo vingi dhidi ya Tehran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *