
Mashirika yasiyo ya kisetikali nchini Tanzania yanalaani vurugu na vitendo vya vikosi vya usalama dhidi ya raia hasa vijana kutoka upinznia kabla wakati na baada ya uchaguzi katika maeneo mbalimbali ya nchini.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Raia wameuawa majumbani mwao kwa “kulipiza kisasi” kwa maandamano ya kupinga serikali ambayo yalikandamizwa kikatili mwishoni mwa mwezi Oktoba nchini Tanzania, mashirika yasiyo ya kiserikali yameshtumu leo Ijumaa, yakilaani “kuenea kwa ukiukwaji wa haki za binadamu kabla, wakati, na baada ya” uchaguzi wa Oktoba 29.
“Video na picha zilizoshirikiwa kwenye mitandao ya kijamii tangu kurejeshwa kwa mtandao zinaonyesha kuenea kwa ulipizaji kisasi mbaya dhidi ya vijana” mashirika saba kutokaTanzania yamesema katika taarifa ya pamoja, moja wapo likilaani kwenye mtandao wa kijamii wa X “raia waliouawa kwa kulipiza kisasi, baadhi waikutwa majumbani mwao.”
Wakati huo huo shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Human Right Watch, HRW, limeshtumu vikosi vya usalama kwa kutumia risasi za moto dhidi ya waandamanaji wa upinzani.
Mamlaka ya Tanzania ilijibu maandamano yaliyoenea baada ya uchaguzi wa Oktoba 29 kwa nguvu kupita kiasi na dhuluma mbalimbali, Human Rights Watch imesema. Mnamo Novemba 1, Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (INEC) inayoshirikiana na serikali ya Tanzania ilitangaza kwamba Rais Samia Suluhu Hassan amechaguliwa tena rasmi kwa asilimia 97.66 ya kura. Mnamo Novemba 3, aliapishwa kwa muhula wake wa pili katika sherehe ambapo raia walipigwa marufuku kuhudhuria, wakati maandamano yalikuwa yakiendelea.
Maandamano hayo, ambayo baadhi yake yaligeuka kuwa ya vurugu, yalianza siku ya uchaguzi na kuendelea kwa siku tatu jijini Dar es Salaam na miji mingine. Polisi walijibu kwa kutumia gesi ya machozi na risasi zamoto kutawanya umati wa watu. Serikali iliweka vikwazo vya intaneti nchini kote mnamo Oktoba 29. Mashirika kadhaa ya ufuatiliaji wa intaneti yalithibitisha kwamba mitambo ya intaneti ilizimwa. Kulingana na ripoti zilizochapishwa jioni ya Novemba 3, ufikiaji wa intaneti ulirejeshwa kwa kiasi fulani, lakini vikwazo kwenye mitandao ya kijamii na majukwaa ya ujumbe vilibaki.