
Angalau watu 54 wamejeruhiwa leo Ijumaa, Novemba 7, kufuatia mlipuko karibu na shule huko Jakarta, mji mkuu wa Indonesia, amesema mkuu wa polisi wa eneo hilo Asep Edi Suheri, bila kutoa maelezo kuhusu chanzo cha mlipuko huo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Kulingana na ripoti za awali, watu wapatao 54 wameathiriwa. Baadhi wana majeraha madogo, wengine ya wastani, na wengine tayari wameruhusiwa kutoka hospitalini,” amesema,akinukuliwa na kito cha televisheni cha Kompas TV.
kiongeza kuwa polisi wamezingira eneo hilo.
Polisi “wanafanya uchunguzi katika eneo la uhalifu,” Asep amesema, akibainisha kuwa timu ya polisi ya kulipua mabomu ya Jakarta ilikuwa mahali hapo ili kubaini chanzo cha mlipuko huo.
Vituo vya huduma ya kwanza vimewekwa katika hospitali mbili ili kusaidia familia kuwapata waathiriwa waliojeruhiwa, pia amesema.
Uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha mlipuko huo, Asep ameongeza. “Tunafanya uchunguzi kwa sababu tukio hili limetokea hivi punde,” amebainisha.