Mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Tanzania yamelaani ripoti za mauaji ya kulipiza kisasi yaliofanywa dhidi ya raia, baadhi wakiwa katika makazi yao wakati wa machafuko ya baada ya uchaguzi.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kauli ya mashirika hayo inajiri wakati huu upinzani kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki ukisisitiza kuwa walinda usalama walitekeleza mauaji ya mamia ya raia.

Rais Samia Suluhu Hassan alitangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 kwa kupata asilimia 98 ya kura zote kwa mujibu wa tume ya uchaguzi.

Rais Samia Suluhu Hassan wakati akiapishwa jijini Dodoma, 03/11/25.
Rais Samia Suluhu Hassan wakati akiapishwa jijini Dodoma, 03/11/25. via REUTERS – PRESIDENTIAL PRESS UNIT

Upinzani kwenye taifa hilo ulizuiwa kushiriki uchaguzi wa urais, ukitaja matokeo ya uchaguzi huo kama kichekesho.

Maandamano yenye vurugu yalizuka kwenye nchini Tanzania siku ya uchaguzi, vyanzo vikithibitisha kuwa idadi kuwa ya watu waliuawa wakati wa vurugu hizo haswa wakati intaneti ilipozimwa.

Polisi wanatuhumiwa kwa kutumia nguvu zaidi dhidi ya waandamanaji
Polisi wanatuhumiwa kwa kutumia nguvu zaidi dhidi ya waandamanaji © Onsase Ochando / Reuters

Kulingana na taarifa ya pamoja ya mashirika hayo ya kiraia, kulikuwa na matumizi makubwa ya nguvu dhidi ya waandamanaji ambao hawakuwa na silaha yakiwemo yale kulipiza kisasi dhidi ya raia wakiwa katika maboma yao.

Aidha mashirika hayo yanasema familia zimeachwa zikiwa na huzuni, watoto pia wakishuhudia wazazi wao wakiteswa.

Mamia ya watu pia wamethibitishwa kukamatwa ambapo hadi sasa baadhi yao wanagali wanashikiliwa na vyombo vya usalama.

Rais Samia amemshtumu machafuko yaliyotokea, na kudai kuwa baadhi ya vijana waliokamatwa kwenye maandamano hayo ni raia wa kigeni,
Rais Samia amemshtumu machafuko yaliyotokea, na kudai kuwa baadhi ya vijana waliokamatwa kwenye maandamano hayo ni raia wa kigeni, REUTERS – Thomas Mukoya

Amos Ntobi, afisa wa chama kikuu cha upinzani Chadema aliliambia shirika la habari la AFP kwamba mamia ya raia walikuwa wameuawa Kaskazini mwa Mji wa Mwanza peke.

“Tuliwaona watu wakipigwa risasi mchana. Kulikuwana miili ya watu mitaani, baadhi ya watu waliuawa hapo kwa hapo wakati wengine wakiachwa wakiwa wamejeruhiwa vibaya sana,” Ntobi aliambia AFP.

“Kuna miili mingi sana kwenye hosipitali.” Alieleza.

Kulingana na Ntobi, hadi kufikia sasa amehudhuria karibia mazishi tisa, mawili yakiwa ni ya watoto wenye umri wa kati ya miaka 9 hadi 11, mmoja akiwa ameuawa karibu na nyumbani kwao wakati mwengine akiuuawa wakati akirejea kutoka dukani.

Vilevile asema kuwa baadhi ya maofisa wa chama chao bado hawajulikani walipo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *