Ukraine imeripoti kulengwa na shambulio jipya la Urusi dhidi ya miundombinu yake ya nishati usiku wa Ijumaa, Novemba 7, kuamkia Jumamosi, Novemba 8, na kusababisha kifo cha mtu mmoja na kukatika kwa umeme katika maeneo kadhaa. Mbali na shambulio dhidi ya Pokrovsk, jeshi la Urusi pia linaongeza mashambulizi dhidi ya vituo vya gesi na umeme kote nchini, na kuzua hofu ya majira ya baridi kali kwa raia huku halijoto ikishuka.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Adui anaanzisha tena shambulio kubwa dhidi ya miundombinu ya nishati ya Ukraine. Kwa sababu hii, kukatika kwa umeme kwa dharura kumetekelezwa katika maeneo kadhaa,” Waziri wa Nishati Svitlana Grinchuk amesema kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.

Tahadhari za mashambulizi ya anga zimetolewa kote Ukraine usiku wa kuamkia Jumamosi, huku mamlaka katika maeneo kadhaa, kuanzia Kharkiv (kaskazini mashariki) hadi Odesa (kusini), zikiripoti mashambulizi yaliyofanywa kwa kutumia ndege zisizo na rubani na makombora, pamoja na mashambulizi dhidi ya vituo vya nishati. Huko Kharkiv, jiji la pili kwa ukubwa nchini, wakazi milioni 1.3 waliamka bila maji, umeme, au joto, kwa wengi wao, anaripoti mwandishi wetu wa ardhini, Emmanuelle Chaze.

Ukrenergo, shirika la serikai linalotoa huduma ya umeme limelazmika kukata umeme katika baadhi ya maeneo kote nchini wakati gridi ilikuwa ikiimarishwa. Miji ya Kyiv, Kremenchuk, na Dnipro pia imeathiriwa sana. Huko Dnipro, mtu mmoja ameuawa na wengine wasiopungua kumi wamejeruhiwa wakati ndege isiyo na rubani iliposhambulia jengo la makazi. Mashambulizi hayo pia yalivuruga sana safari za treni, huku vituo  kadhaa kati ya miji mikubwa vikiripoti kuchelewa kwa saa kadhaa—ingawa safari za treni nchini Ukraine, hadi sasa, zillikuwa imara kwa zaidi ya miaka mitatu ya vita.

Asubuhi ya leo, lengo la Urusi msimu huu wa baridi lilikuwa wazi zaidi: kuzoofisha gridi ya nishati na mifumo ya usafiri nchini Ukraine, njia ya Moscow kuifanya Ukraine isiweze kukaliwa na kujaribu kuiweka katika hali nzito zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *