
Hali ya kutisha inajitokeza mashariki mwa Ukraine, huko Pokrovsk, katika jimbo la Donetsk. Pokrovsk, jiji lenye watu 60,000 kabla ya vita, limekuwa ngome ya upinzani wa Ukraine katika eneo hilo, ambalo vikosi vya Moscow vimekuwa vikijaribu kuliteka kwa miezi kadhaa. Kwa siku kadhaa, shinikizo la Urusi dhidi ya jiji hilo limeongezeka, na Wanajeshi wa Ukraine wanaonekana kuwa karibu kujisalimisha.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Baada ya zaidi ya mwaka mmoja wa kupigania udhibiti wa Pokrovsk, mashariki mwa Ukraine, vikosi vya Urusi vinaonekana kuwa tayari kudhibiti kitovu hiki muhimu cha vifaa kwa jeshi la Ukraine, ambalo limeanzisha operesheni za kuwafukuza.
Baada ya miezi mingi ya kusonga mbele polepole katika pande tatu kuelekea Pokrovsk, jeshi la Urusi limeweza, kuanzia mwezi Septemba, kuingiza vikosi vidogo vikivunja ulinzi wa Ukraine. Wakati huo huo, ndege zisizo na rubani za Urusi polepole ziliweza kushambulia njia zote za usambazaji chakula kwa wanajeshi wa Ukraine hadi kwenye ngome ya Ukraine, hali ambayo tayari iliilazimisha Kyiv kuondoka katika eneo la mpaka la Kursk mnamo mwezi Februari na Machi 2025.
Hali “ngumu”
Ukraine imepeleka vikosi vya ziada katika eneo hilo, ikiwa ni pamoja na vitengo maalum vya jeshi, lakini juhudi hizi “huenda zisitoshe,” mtaalamu wa mauala ya kijeshi kutoka Marekani Michael Kofman amebainisha kwenye mtandao wa kijamii wa X. Siku ya Ijumaa, Novemba 7, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alielezea hali hiyo kama “ngumu,” ikiwa na “mashambulizi 220 dhidi ya Pokrovsk katika siku tatu.” Kulingana na rais wa Ukraine, wanajeshi 314 wa Urusi wameingia katika jiji hilo, wakisaidiwa na kundi lingine la wanajeshi nje kidogo ya mji huo.
Kwa mujibu wa jenerali wa zamani wa Ufaransa na mwanamkakati Olivier Kempf, kurudi kwao katika eneo la Pokrovsk kunaweza kuwa na matokeo mabaya kwa kipindi chote cha vita. “Jambo linalotia wasiwasi zaidi ni kile kilicho upande wa magharibi, yaani mikoa miwili inayowatenganisha Ukraine na Mto Dnieper, ambao hutiririka kutoka Kyiv hadi Bahari Nyeusi. Huko, huna vilima zaidi, hakuna makazi muhimu zaidi ambayo Waukraine wanaweza kushikilia. Kwa hivyo, Urusi itakuwa na aina ya uhuru wa ujanja kati ya kuendelea kusonga mbele kuelekea kaskazini, kuelekea Kramatorsk, na kisha pengine kusonga mbele kuvuka uwanda wa magharibi kuelekea Dnipro, ili kupata udhibiti wa maeneo mengi,” amielezea RFI.