
Katika taarifa iliyotolewa siku ya Alhamisi, Novemba 7, 2025, Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa “inawataka raia wa Ufaransa waweze kupanga kuondoka kwa muda nchini Mali haraka iwezekanavyo,” ikiwashauri kuepuka “kusafiri kwa kutumia njia ya ardhi,” kwani mji mkuu, Bamako, na maeneo mengi ya nchi yanakandamizwa polepole na kizuizi cha wanajihadi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ufaransa inawaomba raia wake nchini Mali “kupanga kuondoka kwa muda” “haraka iwezekanavyo wakitumia ndege za kibiashara ambazo bado zinapatikana.” Hadi sasa, Paris ilikuwa imependekeza tu umakini mkubwa. Katika siku za hivi karibuni, balozi zingine zimewahimiza raia wao kuondoka haraka iwezekanavyo kutokana na hali mbaya ya usalama na uhaba wa mafuta unaosababishwa na wanajihadi wa JNIM (kundi linalodai kupambana kwa ajili ya Uislamu na Waislamu), wanaohusishwa na Al Qaeda. Hii ndiyo hali halisi kwa Marekani, Canada, Ujerumani, na Uingereza.
“Kwa wiki kadhaa, hali ya usalama imekuwa ikizorota nchini Mali, ukiwemo mji mkuu wa Bamako,” ripoti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa (Quai d’Orsay) inabainisha.
Raia 4,300 wa Ufaransa
Mnamo Novemba 6, msemaji wa wizara hiyo, Pascal Confavreux, alisisitiza kwamba Ufaransa ilikuwa ikifuatilia hali ya usalama inayozorota nchini Mali “kwa umakini mkubwa na wasiwasi mkubwa.” Kwa sasa, “utaratibu wa kidiplomasia bado haujabadilika, huku milango ya ubalozi wa Ufaransa ikiwa inafungliwa, ubalozi huo unasimamiwa na mwakilishi, ambaye ni afisaa mwandamizi ambaye ana jukumu kubwa la ulinzi wa kibalozi wa raia wetu 4,300 waliosajiliwa kwenye orodha ya kibalozi,” amesema. “Usalama ndio kipaumbele,” alibainisha.
Mnamo Novemba 4, diplomasia ya Ufaransa iliwataka raia wake “kuwa macho zaidi.”