Maseneta nchini Marekani, wamekubaliana kusitisha mkwamo wa huduma za serikali, ambao umeendelea kwa siku 40, baada ya kukubaliana kupitisha bajeti ya kuruhusu shughuli za kawaida kurejea.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Maelewano haya yamekuja, baada ya Maseneta wa chama cha Democratic na Republican kuafikiana, baada ya mashauriano ya muda mrefu.

Vyombo vya Habari nchini Marekani viongozwa na CNN na Fox News, vinaripoti kuwa, Maseneta hao wamekubaliana kupitisha bajeti ya kufadhili shughuli za serikali, ikiwemo kuwalipa watumishi wa umma mishahara hadi mwezi Januari mwaka ujao.

Aidha, ripoti zinasema Maseneta wanane wa chama cha Democratic, wataunga mkono bajeti ya rais Donald Trump kutoka kwenye chama cha Republican, ambacho kina idadi kubwa ya wawakilishi kwenye Bunge hilo.

Sintofahamu kati ya vyama hivyo hivyo viwili, imesababisha huduma za serikali kukwama, ikiwemo kusitishwa kwa safari za ndege wiki iliyopita.

Maseneta wa chama cha Democratic tangu mwezi Oktoba, walikataa kupitisha bajeti, kama shinikizo kwa rais Donald Trump, kuongezka ruzuku, ili kuendelea kufadhiliwa kwa mpango wa afya kwa wote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *