Akizungumza katika misa hiyo iliyofanyika leo asubuhi Mhashamu Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, amesema taifa limepoteza heshima.

Askofu Ruwa’ichi amesema haki ndiyo msingi wa amani, akisisitiza kwamba amani haiwezi kupatikana pasipo kuwa na haki. “Taifa letu limejeruhiwa, taifa letu limepoteza heshima kutokananna yale yaliyotokea wakati wa uchaguzi mkuu, na sio tu limepoteza heshima, bali limepoteza watu, katika simulizi tulizonazo ni kuwa wako watu walioandamana lakini adhabu ya kuandamana sio risasi,” alisema Askofu Ruwa’ichi.

Taarifa za awali mara baada ya vurugu za Oktoba 29 zinaonesha kuwepo kwa vifo na uharibifu mkubwa wa mali, na hilo lilithibitishwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika hotuba yake ya kwanza baada ya kula kiapo. Huku mashirika mbali mbali ya kimataifa ikiwemo Umoja wa Mataifa,mashirika ya haki za binadamu na chama cha upinzani Chadema wakisema watu wengi wameuwawa.

Tanzania 2025 | Muumini wa Kikatoliki aliyepoteza ndugu katika maandamano wakati wa ibada
Muumini wa Kikatoliki aliyepoteza ndugu katika maandamano wakati wa ibadaPicha: Ericky Boniphace/DW

Madhara haya upotevu wa roho za watu  ndiyo yaliyowaibua wadau wa asasi za kiraia, za kijamii na wanasiasa ambao tangu kutokea kwa maafa hayo wamekuwa wakitoa matamko mbalimbali kulaani ama kukemea vurugu hizo. 

Na leo, Askofu Ruwaichi, wakati wa misa ya wafu amezungumzia  zaidi vifo hivyo akisisitiza kuhusu umuhimu wa haki. Mnamo  Novemba 7, Jeshi la Polisi lilitoa taarifa kuhusu madhara hayo sambamba na vifo lakini likaonya kwa wale wenye mipango ya kufanya vurugu.

Wakati Askofu Mkuu Ruwaichi akiyasema hayo, kwa upande wake Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini, Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo, amesema vurugu katika Taifa lolote hazijawahi kuleta amani, akirejea machafuko yaliyoshuhudiwa katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29.

Tanzania 2025 | Waumini wa Kikatoliki
Waumini wa Kikatoliki wakiombea watu waliouawa wakati wa maandamanoPicha: Ericky Boniphace/DW

“Tunahitaji kumsihi Mungu sanayasitokee tena katika nchi yetu, yasitokee tena, niombe tu kwa unyenyekevu wote kwa ajili ya mustakabali wa taifa letu sote, kuwahimiza na kuzihimiza mamlaka zote, kutafakari sana juu ya haya yaliyotokea”

Shoo ameyasema hayo wakati wa ibada maalum ya kumpongeza Mchungaji Solomon Massawe, aliyestaafu kwa heshima baada ya miaka 34 ya utumishi, iliyofanyika jana Novemba 9, 2025.

Wachambuzi wa masuala ya Amani na diplomasia wamesema katika haya yaliyotokea, Tanzania ina cha kujifunza. Dr Revocatus Kabobe, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria amesemamakundi yote ya watanzania yameathirika na vurugu hizo na hivyo ni wakati wa kufanya mazungumzo. Ibada za Jumapili zilifunikwa na mahubiri yaliyokuwa yakilenga kuhusu Amani, maridhiano na madhara yaliyosababishwa na vurugu za Oktoba 29 wakati wa uchaguzi Mkuu wa Tanzania,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *