Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, limeanzisha kampeni ya kuwahimiza waasi wenye asili ya Rwanda FDLR, kuweka silaha chini, na baadaye kurudishwa katika nchi yao, kwa mujibu wa maelewano ya kusitisha vita Mashariki mwa nchi hiyo, yaliyotiwa saini, jijini Washington Juni 27.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, FDLR wanapinga mpango huo na wanataka mazungumzo na serikali ya Kigali.

Kampeni hiyo imelenga haswa wilaya ya Walikale Katika mkoa wa Kivu kaskazini mashariki mwa Congo ambapo, Polisi na vikosi vya jeshi la DRC vina hamasisha waasi wa FDLR kwa kutumia Matangazo ya redio na helikopta pia.  

Ado Laurent Kasongo ni kiongozi wa eneo hili.

“Tunapozungumza juu ya FDLR siwezi kukataa! ikiwa kuna idadi ya watu ambao wanajua wengine pale walipo, ni wakati wakuwahamasisha ili warudi  majumbani kwao au kwenda kwa MONUSCO au mbele ya FARDC ili warudi majumbani kwao na amani” alisema Ado Laurent Kasongo.

Viongozi wa madhehebu mbalimbali na asasi za kiraia WALIKALE wamehusika katika kuhamasisha kujisalimisha kwa waasi wa FDLR.

Wanajeshi wa Tume ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa nchini DRC Monusco
Wanajeshi wa Tume ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa nchini DRC Monusco © Moses Sawasawa / AP

Jaitro Luand ni Mmmoja wa viongozi wa Mashirika ya Kiraia mkoani Kivu Kaskazini.

“Mwaka wa 1998 hadi leo watu wanakufa kiholela, akina mama wanabakwa, nyumba zinateketezwa, vitu vingi vinaporwa, ni kwa sababu ya hawa watu. Upande wangu hili likifanyika kwa kwelii bila mchezo linaweza kuleta amani WALIKALE na kumaliza mizozo Kivu kaskazini.” Alisema Jaitro Luand.

Serikali ya Rwanda imekuwa ikiituhumu DRC kwa kushirikiana na waasi wa FDLR, madai ambayo Kinshasa imekanusha.

TSCHUBE NGOROMBI Goma RFI KISWAHILI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *