Kinshasa imeanzisha kampeni ya kuwataka waasi wa FDLR kuweka chini silaha na kujisalimisha kwa jeshi au kikosi cha MONUSCO, ikiwa na lengo la kuwarejesha nchini Rwanda.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na taarifa ya mamlaka ya Kinshasa, iwapo waasi hao watakosa kufanya kama wanavyotakiwa, watalazimishwa.

Hatua hii inaelezwa kuchukuliwa chini ya makubaliano ya tarehe 27 mwezi Juni kati ya  wajumbe wa serikali ya Kinshasa na Kigali walipokutana jijini Washington.

DRC na Rwanda zilipitia maandalizi ya oparesheni za kijeshi dhidi ya waasi wa FDLR tarehe 7 ya mwezi Novemba na kuafikia makubaliano ya utekelezwaji wa makubaliano hayo.

Watu waliotajwa kuwa waasi wa FDLR wakikaguliwa na polisi wa Rwanda kwenye mpaka wa Goma, Machi 1, 2025.
Watu waliotajwa kuwa waasi wa FDLR wakikaguliwa na polisi wa Rwanda kwenye mpaka wa Goma, Machi 1, 2025. © Jospin Mwisha/AFP

Kwa upande wake, uongozi wa kundi hilo la FDLR akiwemo msemaji wao Luteni Kanali Octavien Mutimura, umeiambia RFI Kifaransa kuwa hauna mpango wa kujisalimisha kwa serikali ya DRC.

“Kwanza, lazima tuangazie chanzo la mapambano yetu. Tuko hapa kujilinda sisi wenyewe pamoja na wakimbizi Wanyarwanda.” Alisema Luteni Kanali Octavien Mutimura, Msemaji wa waasi wa FDLR-FOCA, amesema

“Kuweka chini silaha bila ya marsharti yanayohitajika kushugulikia ni suala lisilowezekana.” Ameongeza.

Waasi wa M23 wakiwa mashariki ya Congo.
Waasi wa M23 wakiwa mashariki ya Congo. AP – Janvier Barhahiga

Aidha FDLR inasema haiogopi kushambuliwa.

“Ukiwa ndani zaidi, hauwezi ukawa na uoga, sisi ni miongoni mwa watu wanaolengwa na Kigali.” alisema Mutimura.

“Tutaendelea kushinikiza hadi Kigali ikubali mazungumzo kati ya watu wa Rwanda pamoja na kurejea kwa heshima kwa wakimbizi.” Aliongeza Luteni Kanali Octavien Mutimura.

Licha ya kutuhumiwa katika ripoti za Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na wanajeshi wa FARDC, FDLR inakanusha kuwepo kwa ushirikiano wowote na wanajeshi wa DRC.

FDLR wanadai kuwa na makao yao katika maeneo yanayokaliwa na waasi wa AFC/M23, maeneo ambapo mara kwa mara huwa kunaripotiwa makabiliano kati ya FDLR na M23 haswa katika maeneo ya Bwisha huko Rutshuru.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *