
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa wagonjwa wasiopungua 16,500 katika Ukanda wa Gaza wanasubiri kupelekwa nje kwa ajili ya matibabu na kusisitiza kuwa suhula zake za tiba ziko tayari mpakani lakini haziwezi kuingia katika eneo hilo kufuatia Israel kufunga vivuko hivyo.
Shirika hilo la Umoja wa Mataifa lenye makao yake makuu mjini Geneva, Uswisi limetoa wito ili kuhakikisha usambazaji mtawalia wa misaada ya kibinadamu kupitia vivuko vyote katika Ukanda wa Gaza, kutokana na kuzorota kwa hali ya afya katika eneo hilo.
WHO imesisitiza kuwa kuna haja kwa nchi nyingine zaidi kuwapokea wagnjwa na majeruhi kutoka Gaza kwa ajili ya matibabu.
Taarifa hiyo imesisitiza kuwa mfumo wa afya katika Ukanda wa Gaza umesambaratika kikamilifu kutokana na vizuizi na uhaba wa vifaa vya matibabu na mafuta.
Shirika la Afya Duniani limesisitiza kuwa maelfu ya watu waliojeruhiwa wanahitaji kufanyiwa upasuaji haraka iwezekanavyo; oparesheni ambazo haziwezi kufanyika ndani ya Gaza.
Wakati huo huo, Umoja wa Maataifa umesema kuwa ukwamishaji wa Israel unaendelea kuzuia usmabazaji wa misaada ya kibinadamu kuelekea Ukanda wa Gaza yapata mwezi mmoja sasa tangu Telv Aviv na harakati ya muqawama ya Palestina Hamas zitekeleze makubaliano ya kusitisha mapigano.
Naye Farhan Haq, msemaji wa Umoja wa Mataifa ameinukuu Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA) na kusema: Juhudi za kuongeza misaada kwa ajili ya watu wa Gazazinaendelea kukwamishwa, washirika wakuu wa misaada ya kibinadamu wamewekewa marufuku, vivuko na njia za kupitisha misaada bado ni chache sana huku ukosefu wa usalama ukishuhudiwa licha ya kufikiwa usitishaji mapigano.