
Mamia ya Waisraeli wamekusanyika hii leo katika mji wa kati wa Kfar Saba kwa mazishi ya afisa wa jeshi Hadar Goldin baada ya Hamas kurejesha mabaki yake zaidi ya muongo mmoja baada ya kifo chake huko Gaza.
Umati wa watu ulifurika katika makaburi hayo ya kijeshi, huku baadhi wakipanda juu ya paa ili kuyashuhudia mazishi hayo na wengine wakifuatilia shughuli hiyo kupitia televisheni zilizowekwa mitaani.
Israeli ilipokea mabaki ya Goldin siku ya Jumapili kama sehemu yamakubaliano yanayoendelea ya kusitisha mapigano Gaza yaliyosimamiwa na Rais wa Marekani Donald Trump.
Hadar Goldin aliyekuwa na miaka 23, aliuawa mnamo Agosti 1, 2014 wakati akiongoza misheni ya Israel huko Gaza ya kuharibu mahandaki ya Hamas huko Rafah na mwili wake kuchukuliwa na Hamas.