Maseneta nchini Marekani wamefikia makubaliano ya kurejesha ufadhili kwa serikali kuu na kukomesha hatua ya ufungwaji wa shughuli za uendeshaji serikali ambazo zimeingia siku yake ya 40hivi leo na kulazimisha operesheni nyingi za serikali kusimamishwa.

Vyombo vya habari nchini Marekani, vikiwemo vituo vya CNN na Fox News, vimeripoti kwamba watunga sheria hao wameafikiana kuruhusu ufadhili kwa serikali kuu hadi mwezi Januari baada ya kubishana sana juu ya ruzuku kwenye huduma za afya, mafao ya chakula na hatua ya Rais Donald Trump kuwafuta kazi wafanyakazi kadhaa wa serikali kuu.

Makubaliano hayo ya leo yanatazamiwa kupigiwa kura naBazara la Senetiusiku wa leo. Hata hivyo, makubaliano hayo yamefikiwa baada ya hasara kubwa sana, hasa kwenye sekta ya usafirishaji, ambapo zaidi ya safari 7,000 zilicheleweshwa jana Jumapili, huku zaidi ya 1,000 zikifutwa mwishoni mwa Juma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *