Kwa mujibu wa ripoti hiyo njia endelevu ya kupooza joto zinaweza kupunguza asilimia 64 ya uzalishaji wa gesi chafuzi unaotokana na mifumo yabaridi ifikapo mwaka 2050, kulinda watu bilioni 3 dhidi ya joto linaloongezeka, na kuokoa hadi dola za Marekani trilioni 43 kutokana na gharama za umeme na miundombinu. Miji 185 imejiunga na mpango wa piga vita joto au Beat the Heat pamoja na nchi 72 zilizosaini  Ahadi ya Ulimwengu ya mfumo wa kupooza joto.

Puto kubwa, yenye urefu wa zaidi ya mita 7, inayowakilisha tani moja ya gesi ya carbon dioxide.

UN/Mark Garten

Puto kubwa, yenye urefu wa zaidi ya mita 7, inayowakilisha tani moja ya gesi ya carbon dioxide.

Belém, 11 Novemba 2025

Katikati ya ongezeko la mawimbi ya joto na mahitaji ya huduma za mifumo ya baridi ya kupooza joyo au viyoyozi, Shirika la UNEP limeonya kuwa bila hatua mpya, mahitaji ya viyoyozi yataongezeka mara tatu ifikapo 2050, na uzalishaji wa gesi chafuzi kufikia tani bilioni 7.2 za CO₂e.

Ripoti hiyo ya Global “Cooling Watch 2025” au ufuatiliaji wa mfumo wa viyoyozi inapendekeza njia endelevu ya mifumo ya kupooza joto inayoweza kupunguza uzalishaji wa hewa chafuzi kwa asilimia 64 na kuokoa trilioni za dola kupitia mbinu za asili, matumizi madogo ya nishati, na teknolojia rafiki kwa mazingira.

Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP, Inger Andersen, amesema huduma za viyoyozi zinapaswa kuchukuliwa kama miundombinu muhimu, akisisitiza kuwa dunia haiwezi kutumia viyoyozi pekee kushinda joto, bali inahitaji suluhu za asili na endelevu ili kulinda watu, uchumi na mazingira.

Njia endelevu za mifumo ya viyoyozi

Ripoti ya Cool Coalition inayoongozwa na UNEP inaonesha kuwa njia endelevu ya kupooza joto inaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa gesi chafuzi na kuboresha upatikanaji wa huduma zaviyoyozi kwa wote bila kuathiri mazingira.

Njia hii inachanganya mbinu za asili, teknolojia zenye matumizi madogo ya nishati, na kupunguza matumizi ya majokofu ya HFC chini ya Mkataba wa Kigali. Takribani theluthi mbili ya upunguzaji wa uzalishajihewa chafuzi  inatokana na suluhu hizi, ambazo ni nafuu na muhimu kwa watu bilioni 3 zaidi kufikia mwaka 2050.

Kwa utekelezaji kamili,ripoti inasema njia hii inaweza kuokoa hadi Dola za Marekani trilioni 17 katika gharama za nishati na kuepusha uwekezaji wa hadi trilioni 26 katika miundombinu ya umeme.

Kukabiliana na ongezeko la joto

Hatua hizi ndizo msingi wa mpango wa Mutirão Contra o Calor Extremo / Beat the Heat, juhudi za pamoja zinazoongozwa na urais wa COP30 wa Brazili na UNEP Cool Coalition zinazolenga kutekeleza ahadi ya ulimwengu ya kupooza joto kwa ngazi ya ndani na kuziba mapengo katika sera, fedha na utekelezaji wa uthabiti wa joto na kupooza mijini.

Mradi wa Makazi ya bei nafuu ya Paa la Baridi huko Perumbakkam, Chennai, umeandaliwa na Taasisi ya Rocky Mountain, Muungano wa Cool unaoongozwa na UNEP na Serikali ya Jimbo la Tamil Nadu.

© UNEP India

Mradi wa Makazi ya bei nafuu ya Paa la Baridi huko Perumbakkam, Chennai, umeandaliwa na Taasisi ya Rocky Mountain, Muungano wa Cool unaoongozwa na UNEP na Serikali ya Jimbo la Tamil Nadu.

Leo, zaidi ya miji 185 kuanzia Rio de Janeiro hadi Jakarta hadi Nairobi na washirika 83 wamejiunga na Beat the Heat sambamba na nchi 72 zilizosaini Ahadi ya Ulimwengu ya Kupooza.

Beat the Heat ni moja ya mipango inayodhihirisha maana ya mutirão, watu kuungana na kufanya kazi kwa uelewa wa pamoja. Hivyo ndivyo mpango huu ulivyo, unaleta hoja kwa njia inayoeleweka na kuleta watu pamoja kufanya kazi ya kweli ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi,” amesema Balozi André Corrêa do Lago, Rais Mteule wa COP30.

Maendeleo yanafanyika lakini kwa kiwango tofauti

Kwa mujibu wa ripoti nchi 72 zimejiunga na ahadi ya ulimwengu ya kupooza joto ili kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi unaotokana na viyoyozi  kwa asilimia 68 kufikia mwaka 2050 kupitia Njia Endelevu ya mifumo ya Kupooza joto.

Kufikia katikati ya mwaka 2025, nchi 29 tayari zimeweka malengo maalum ya kupunguza uzalishaji katika sekta ya kupooza, huku 5 zingine zikiwa katika hatua za maendeleo.

Kwa jumla, Ripoti hiyo imebainisha kuwa nchi 134 zimejumuisha suala la mifumo ya kupooza joto katika michango yao iliyokusudiwa Kitaifa (NDCs), Mipango ya Kitaifa ya Urekebishaji (NAPs), Mikakati ya muda mrefu ya maendeleo chini ya uzalishaji (LT-LEDS), au mipango mingine ya nishati na tabianchi.

Hata hivyo, ni nchi 54 pekee zenye sera kamili zinazohusisha maeneo matatu muhimu ya mifumo ya kupooza joto:

1. Kupooza joto kwa njia za asili kupitia kanuni za ujenzi,

2. Viwango vya chini vya utendaji wa nishati (MEPS), na

3. Mabadiliko ya majokofu yanayotumika.

Nchi 78 zinashughulikia nguzo mbili kati ya hizo, 40 zinashughulikia moja pekee, na 20 bado hazijaanza.

Pengo kubwa zaidi lipo katika nchi za Afrika na Asia-Pasifiki, ambako ongezeko kubwa la mahitaji ya mifumo ya kupooza joto linatarajiwa.

Ripoti inatoa mapendekezo kadhaa ili kuongeza kasi ya utekelezaji, yakiwemo:

·        Kuhama kutoka katika hatua za dharura kwenda kwenye utawala wa kimfumo na wa viwango vingi kuhusu joto kali na huduma za mifumo ya kupooza joto.

·        Kutambua ulinzi dhidi ya joto na huduma za viyoyozi kama mali ya umma.

·        Kipaumbele kwa suluhu za asili na za kijamii ikiwemo usanifu wa mijini ili kupunguza mzigo wamifumo ya viyoyozi, kupunguza athari ya kisiwa cha joto mijini, na kupunguza shinikizo kwenye gridi za umeme.

UNEP inaisaidia serikali kujumuisha vipengele vya kupoeza tulivu - kama vile uingizaji hewa wa asili na kuta za maboksi - kwenye miradi ya nyumba ya bei nafuu.

© UNEP India

UNEP inaisaidia serikali kujumuisha vipengele vya kupoeza tulivu – kama vile uingizaji hewa wa asili na kuta za maboksi – kwenye miradi ya nyumba ya bei nafuu.

Kauli za wadau

Kama msaini wa Ahadi ya Ulimwengu ya Kupooza, Singapore inachukua hatua thabiti kuelekea utekelezaji wa ahadi hiyo na inajivunia kusaidia mpango wa Beat the Heat kwa kushiriki utaalamu wetu wa kiufundi na uzoefu katika mifumo endelevu ya viyoyozi na udhibiti wa joto mijini. Tutaleta pamoja wawakilishi wa Ahadi ya Ulimwengu ya Kupooza, watunga sera na wataalamu kutoka duniani kote kwa mapitio ya maendeleo na kujadili suluhisho bunifu. Singapore pia itashiriki uwezo wetu wa kiteknolojia kupitia Digital Urban Climate Twin kusaidia miji duniani kutabiri na kupunguza joto la mijini. Hii inaonesha dhamira yetu ya kuendeleza suluhu shirikishi kwa mustakabali baridi na thabiti wa tabianchi.”  Amesema Mhe. Grace Fu, Waziri wa Uendelevu na Mazingira, Singapore

Dkt. J. Jeyaranjan, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Mipango ya Jimbo, Serikali ya Tamil Nadu ameeleza pia kuwa,kutoka hatua ya awali ya kutangaza joto kama janga maalum la jimbo hadi kuandaa Mipango ya Hatua dhidi ya Joto kwa miji mikubwa, Tamil Nadu imeanzisha mfano wa kina wa utawala wa joto.

Kwa kuungana na jumuiya ya kimataifa kupitia mpango wa Beat the Heat, tunapata nafasi ya kujifunza kutokana na uzoefu wa wengine huku tukishiriki mbinu zetu za utawala zinazotegemea takwimu. Ushirikiano huu wa kujifunza utasaidia miji yote inayoshiriki kuwa thabiti, shirikishi na tayari kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Fortaleza inaweka maumbile katikati ya mikakati yetu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Tumejitolea kupanua wigo wa maeneo ya kijani na bustani ndogo zinazopunguza joto na kulinda walio hatarini zaidi. Hii ni kuhusu usawa, afya na ubora wa maisha na kupitia Beat the Heat tunataka kushiriki na kujifunza na miji mingine nchini Brazili na duniani ili kuharakisha mabadiliko haya.” Amesisitiza  Mhe. Evandro Leitão, Meya wa Fortaleza, Brazili

Na Luteni Jenerali Bashir Mohamed Jama, Waziri wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi wa Somalia anaeleza kuwa kwa miji ya Somalia kama Dolow, Baidoa, Galkaio na Bossaso, mifumo endelevu ya viyoyozi si anasa  ni uhai. Kwa kujiunga na Beat the Heat na kushirikiana na Cool Coalition inayoongozwa na UNEP, wanalenga kulinda maisha na riziki dhidi ya joto linaloongezeka huku wakitekeleza ahadi zao za tabianchi. Pamoja na miji mingine, wanaweza kugeuza mbinu za asili za mifumo ya upoozaji na ubunifu kuwa uimara wa kweli kwa jamii zao zilizo hatarini zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *