Nchi ya Ufaransa, hivi leo ilifanya kumbukizi ya miaka 10 tangu kutekelezwa kwa shambulio baya zaidi la kigaidi jijini Paris, ambapo watu zaidi ya 130 waliuawa.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kumbukizi hiyo iliongozwa na rais Emmanuel Macron, aliyekuwa ameambatana na mke wake Brigitte pamoja na maofisa wengine wa juu katika serikali yake akiwemo rais wa zamani Francois Hollande, ambaye alikuwa katika uwanja wa Stade de France wakati shambulio likitekelezwa.
Wanajihadi wa kiislamu waliuawa watu 130 kwa kuwapiga risasi pamoja na kujilipua ndani na nje ya jiji la Paris usiku wa Novemba 13 mwaka 2015, kundi la Islamic State likikiri kuhusika kwenye mashambulio hayo.

Washambuliaji waliwaua watu 90 katika ukumbi wa maonesho wa Bataclan, ambako bendi ya Marekani ya Eagles of Death Metal ilikuwa ikitumbuiza, watu wengine wakiuawa katika migahawa tofauti jirani na uwanja wa Stade de France ambako mashabiki walikuwa wakitazama mechi kati ya Ufaransa na Ujerumani.
Katika tukio hilo mwanajihadi mmoja pekee alikamatwa kwa jina la Salah Abdeslam, ambaye sasa anatumikia kifungo cha maisha jela, wanajihadi wengine 9 wakijilipua au kuuawa na polisi.
Rais Macron na Hollande kwa nyakati tofauti wamelaani mashambulio hayo na kuvitaka vyombo vya usalama kutoruhusu yajirudie tena.