
Watu zaidi ya 20 wameuawa Wilayani Lubero nhcini DRC, wakiwemo wagonjwa 17 waliokuwa wamelazwa katika hospitali mjini Biambwa usiku wa kuamkia leo, umbali na kilomita 90 Magharibi mwa mji wa Butembo. Waasi wa ADF wanatuhumiwa kutekeleza mauaji hayo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Shambulio hilo lilitekelezwa katika kituo cha afya na makaazi ya raia huku Biambwe. Baadhi ya wahudumu wa afya wakiripotiwa kutekwa na waasi hao.
Macaire Sivikunula ni kiongozi wa sekta ya Bapere wilayani Lubero.
“ADF waliwasili usiku katika kituo ya afya ambapo wamewauwa wagonjwa na kuiba dawa.” Alisema Macaire Sivikunula.
Raia wa Lubero wamehuzunishwa na kitendo hiki cha ADF. Samuel kagheni ni makaazi wa sekta ya Bapere.
“Serikali inastahili kutilia nguvu suala la usalama. Huko Wilayani Masisi wanatumia ndege kuwapiga M23. Ni kwa nini hizo ndege zisitumiwe kushambulia ngome za ADF.” Alisema Samuel kagheni ni makaazi wa sekta ya Bapere.
Raia wengine 18 waliuwa na waasi hao wa ADF na washirika wao Oktoba 18 .
Eriksson LUHEMBWE Beni RFI Kiswahili .