Kwa mujibu wa taarifa ya UNIFIL, risasi nzito zilitua umbali wa takriban mita tano kutoka kwa walinda amani waliokuwa wakitembea kwa miguu, na kuwafanya walazimike kujificha katika eneo hilo kwa usalama.

UNIFIL imesema kuwa walinda amani walitumia njia rasmi za mawasiliano kuiomba Israel kusitisha mashambulizi. Baada ya takribani nusu saa, tanki la Merkava lilirudi ndani ya kituo cha jeshi la Israel, na walinda amani waliweza kuondoka salama.

Hakuna majeruhi walioripotiwa.

Kwenye taarifa hiyo, UNIFIL imesisitiza kuwa tukio hilo ni ukiukaji mkubwa wa Azimio namba 1701 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Kikosi hicho kimerejea wito wake kwa Jeshi la Israel “kusitisha mara moja vitendo vyovyote vya uchokozi au mashambulizi yanayolenga au kutokea karibu na walinda amani,” ambao wanaendelea kusaidia juhudi za kurejesha utulivu ambao Israel na Lebanon wamesema wanaudhamini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *