Angalau watu thelathini walifariki bada ya kuporomoka kwa daraja katika eneo la madini la Kalando, yapata kilomita arobaini kutoka Kolwezi, katika mkoa wa Lualaba, nchini DRC. Tukio hilo lilitokea siku ya Jumamosi, Novemba 15. Idadi hii ya vifo inabaki kuwa ya muda katika hatua hii huku utafutaji wa watu waliotowea ukiendelea.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wengi wa waathiriwa walikuwa wachimbaji madini kwa kutumia mfumo wa kienyeji. Kalando ni mgodi wa shaba wa nusu viwanda. Ukiwa katika kijiji cha Mulondo, katika eneo la Mutshatsha (kusini-mashariki mwa DRC), unaendeshwa na wachimbaji wanaotumia mfumo wa kienyeji na kundi la uchimbaji wa Pajeclem, chini ya ulinzi wa kijeshi.

Wakati mamlaka katika mkoa wa Lualaba zikiripoti idadi ya vifo ya 34, sawa na idadi ya miili iliyopatikana na kupelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti, chama cha wachimbaji wanaotumia mfumo wa kienyeji wa eneo hilo kinatoa takwimu ya juu zaidi: 49 wamefariki na makumi kadhaa hawajulikani walipo.

Katika hatua hii, sababu za mkasa uliotokea siku ya Jumamosi asubuhi bado hazijaeleweka, huku maelezo kadhaa yakitolewa. “Licha ya marufuku rasmi ya kuingia kwenye eneo hilo kutokana na mvua kubwa na hatari ya maporomoko ya ardhi, wachimbaji haramu hao waliingia kwenye machimbo kwa nguvu,” anasema Roy Kaumba Mayonde, Waziri wa Mambo ya Ndani wa mkoa, katika taarifa kwa vyombo vya habari siku ya Jumapili, Novemba 16. “Kuingia kwa haraka” kwa wachimbaji hao kulisababisha kuporomoka kwa daraja la muda walilokuwa wamejenga ili kuvuka mtaro uliojaa maji unaonyesha mpaka wa eneo hilo, ameongeza.

Mzozo kati ya wachimbaji na wanajeshi

Lakini kulingana na vyanzo kadhaa miongoni mwa wachimbaji wanaotumia mfumo wa kienyeji na mashirika ya kiraia huko Lualaba, janga hilo linawezekana zaidi kutokana na hofu iliyosababishwa na wanajeshi waliohusika na kulinda eneo la madini. Kufuatia mabishano, wanajeshi hao wanaripotiwa kuwafyatulia risasi wachimbaji hao ili kuwatawanya. “Wachimbaji waliendelea kuwasili: hapo ndipo walipoanza kupiga risasi. Na kisha kulikuwa na machafuko! Katika hali ya kila mtu kujaribu kuokoa maisha yake, watu wengi waliishia kukanyagana,” anasimulia mmoja wao, huku mwingine akisema: “Askari walitushambulia ingawa walipokea nusu ya uzalishaji wetu. Sasa, tunapaswa kuwaambia waondoke na waache kuchukua mali yetu. Hatutakubali!”

Gavana wa mkoa wa Lualaba, Fifi Masuka, anabainisha kwamba kila kitu kinafanywa ili kuwasaidia waathiriwa na kuelewa jinsi ajali hiyo ilivyotokea. “Maporomoko ya mlima yanaweza kuwa sababu: mvua kubwa ilisababisha ardhi kuteleza […]. Kama nilivyosema, uchunguzi unaendelea, na watakaohusika na tkio hilo, sheria itafuata lkono wake,” amesema.

Wakati watu wengine kadhaa wakiaminika bado wamefukiwa kwenye mgodi, kulingana na mashirika ya kiraia, ujumbe kutoka serikali ya mkoa na idara ya Huduma za Dharura na Usaidizi wa Uchimbaji Madini kwa kutumia mfumo wa kienyeji na wa kiwango cha chini (SAEMAPE) ulizuru eneo hilo. Wakati wa ziara hii, mamlaka za eneo hlo zimebainisha kuwa utafutaji wa waliopotea utaendelea. Pia walitangaza kusitishwa kwa shughuli za uchimbaji madini katika eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *