Nchini Mali, hali ya usalama bado inatia wasiwasi, hasa kusini mwa nchi. Huko Loulouni, kilomita hamsini tu kutoka mpaka wa Côte d’Ivoire, makabiliano yanafanyika kati ya magaidi wa JNIM na wawindaji wa jadi wa Dozo. Kutokana na vurugu hizi, familia nyingi zimelazimika kutoroka makazi yao. Watu mia kadhaa tayari wamepata hifadhi kaskazini mwa Côte d’Ivoire katika siku za hivi karibuni.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Abidjan, Abdoul Aziz Diallo

Wimbi la wakimbizi wa Mali wanatorika makazi yao na kukimbia nchini Côte d’Ivoire, haswa katika eneo la Tchologo. Ni vigumu kutathmini ukubwa wa wimbi hilo kwa wakati huu: “Shughuli za sensa zimeanza tu,” anasema mfanyakazi kutoka shirika moja la kutoa misaada ya kibinadamu. Lakini huko Pogo, mji wa mpakani, zaidi ya watu 200 wamewasili katika siku chache tu, hasa wanawake na watoto. Mamlaka za eneo hilo na wakazi wanajaribu kujipanga licha ya rasilimali chache, kama kiongozi huyu wa vijana huko Pogo anavyoshuhudia.

“Kijiji kimezidiwa na idadi ya wakimbizi”

“Mamlaka yakKijiji imewapa mifuko michache ya mchele na pesa. Lakini haitoshi. Malazi ni magumu; kijiji kwa sasa kina idadi kubwa ya wakimbizi. Baadhi wamepewa hifadhi katika vibanda vidogo, wengine wanalala nje. Kwa bahati nzuri, ni msimu wa kiangazi; bado hakuna mvua. Lakini hali hii ni ngumu,” amesema. Kutokana na hali hii, Baraza la Usalama la kitaifa la Côte d’Ivoire limeamuru kuwaorodhesha wanaotafuta hifadhi na kumuomba Mkuu wa Jeshi kuimarisha usalama katika mipaka ya kaskazini.

Dola milioni moja zimetengwa

Kulingana na UNHCR, Côte d’Ivoire tayari inawapa hifadhi karibu watafuta hifadhi 70,000, wengi wao kutoka nchi jirani ya Burkina Faso, ambayo pia imeathiriwa na vurugu za kigaidi. Vituo viwili vya mapokezi vimejengwa na mamlaka, lakini wengi wa wakimbizi hawa wanahudumiwa na familia zinazowapa hifadhi. Mapema wiki hii, Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) ilizindua mpango wa usaidizi wa kibinadamu kwa watafuta hifadhi, wakimbizi, na jamii zinazowapa hifadhi. Bajeti ya dola milioni moja imetengwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *