Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Anicet-Georges Dologuélé na Henri-Marie Dondra walielezea faraja yao: baada ya miezi kadhaa ya uvumi kuhusu kutostahiki kwao, mawaziri wakuu hao wawili wa zamani wamejikuta faili zao za kugombea zikiidhinishwa  na Baraza la Katiba kwa uchaguzi wa urais wa Desemba 28, 2025. Uamuzi ambao waangalizi na wadau wengi wanauelezea kama wa kisiasa, badala ya kisheria.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu maalum huko Bangui, François Mazet

“Lazima tuwe tayari kugeuza sheria ili kulinda amani”: hivi ndivyo msemaji wa walio wengi wa katika kambi ya rais katika Bunge la taifa, Mathurin Dimbélé Nakoé, alivyoelezea kwa ufupi kwenye RFI maoni ya wafuasi wa Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Faustin-Archange Touadéra, baada ya kuidhinishwa kwa wagombea wa wawili wakuu wa upinzani wakuu dhidi ya mkuu wa nchi.

Ingawa Anicet-Georges Dologuélé na Henri-Marie Dondra wamekuwa wakichoka kuonyesha kesi zao kwa hoja za kisheria kila mara, mmoja wa waangalizi anasema: “Kama wanliruhusiwa kugombea, ni kwa sababu Touadéra alitaka iwe hivyo.”

Kwa mtazamo wa kijamii na kisiasa tu, hili ni jambo zuri kwa sababu Jamhuri ya Afrika ya Kati imepiga hatua kubwa. Migogoro yote iliyotokea ilitokana na maandamano, ama kuhusu wagombea au matokeo ya uchaguzi. Nadhani Baraza la Katiba limetuzuia kurudi kwenye matatizo yale yale ya zamani. Hilo ni kwa mtazamo wa kijamii na kisiasa tu. Sasa, kwa mtazamo wa kisheria, kuna tatizo kwa sababu vifungu vya Katiba vinavyohusiana na uchaguzi wa urais vimepuuzwa, hasa sharti kwamba, ili kuwa mgombea wa wa kiti cha urais, mtu lazima awe na uraia wa Jamhiri ya Afrika ya Kati pekee. Hata hivyo, inadhihirika kuwa Bw. Dologuélé alikiri kwamba alipoteza uraia wake wa Jamhuri ya Afrika ya Kati mwaka wa 1994 na kuwa raia wa Ufaransa, na Bw. Dondra ana uraia pacha. Yeye ni Mkongo (DRC) na pia raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Kama unavyoona, kutoka kwa mtazamo wa kisheria kabisa, hii inaleta tatizo. Lakini kutokana na hali ambayo nchi ilikumbwa kwa miongo kadhaa, lazima tuwe tayari kupotosha sheria ili kulinda amani.

Katika taarifa, chama cha Movement for the Liberation of the Central African People (MLPC) cha Martin Ziguélé, ambacho kimechagua kususia uchaguzi, kinalaani “mchezo wa kuigiza” kutoka Baraza la Katiba.

“Kuwaomba radhi wafadhili” wanaofadhili uchaguzi

Vyanzo kadhaa vinabaini kwamba, kwa kufuata taratibu zilizowekwa, watu hao wawili wangeweza kuondolewa. Vyanzo hivi pia vinaona uamuzi huu kama njia ya “kuwaomba radhi wafadhili,” wanaofadhili uchaguzi na walikuwa wakishinikiza uchaguzi jumuishi.

Mamlaka ya kitaifa ya Uchaguzi (ANE) inahakikisha kwamba itakuwa “tayari” siku ya uchaguzi; kadi za wapiga kura zilipokelewa siku ya Alhamisi.

Mnamo Novemba 14, Baraza la Katiba lilitangaza orodha ya mwisho ya wagombea saba wa uchaguzi wa urais wa Desemba 28, 2025, wakiwemo Rais Faustin-Archange Touadéra na Mawaziri Wakuu wa zamani Henri-Marie Dondra na Anicet-Georges Dologuélé. Rufaa zote za kutostahiki zilizowasilishwa dhidi yao zilikataliwa na Baraza la Katiba. Wagombea wengine watatu walikataliwa, haswa kwa ukosefu wa hati miliki za mali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *