Ulaya inasema haiko tayari kwa shambulio kubwa la ndege zisizo na rubani za Urusi na lazima iunganishe uwezo wa Ukraine chini ya hatari ya kufanya “kosa la kihistoria,” Kamishna wa Ulinzi wa Ulaya Andrius Kubilius amesema leo Jumatatu, Novemba 17. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Hatuko tayari kukagua na kuangamiza ndege zisizo na rubani za Urusi,” amesema akisikitika katika hotuba huko Vilnius. “Urusi inajifunza haraka. Na sisi?” ameuliza. 

Vita nchini Ukraine vimebadilisha sheria za vita, amebainisha. “Vita vya kesho havitashindwa kwa vifaru na mizinga, bali kwa ndege zisizo na rubani na makombora,” ametangaza, akitaka kujifunza kupitia uzoefu wa Ukraine, kulingana na shirika la habari la AFP.

Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Andrii Sybiha, ametoa wito kwa wanaowaunga mkono kuchangia fedha ili kuongeza uzalishaji wa droni.

Amesema kuwa sekta ya ulinzi ya Ukraine inahitaji fedha ili kufanikisha hilo, akiongeza kwa kusema wanaweza kutengeneza hadi droni milioni 20 mwaka ujao ikiwa watapata ufadhili wa kutosha. Katika andiko lake la Jumapili kwenye mtandao wa kijamii wa X amesema Rais wa Urusi, Vladimir Putin, ataacha vita ikiwa masharti mawili yatatimizwa: “Kwaanza vita vitaisha tu pale Urusi itakapoona kuwa kushinda haiwezekani na pili kubaini kuwa kuendelea kupigana kunagharimu zaidi kuliko kuikomesha.”

Ukraine imekuwa ikizalisha maelfu ya droni mbalimbali kwa miezi kadhaa. Urusi na Ukraine zote zinatumia droni kwa wingi katika mapambano yao, hata hivyo, hakuna upande unaotoa takwimu kamili za uzalishaji wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *