Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Bangladesh, Sheikh Hasina, amepatikana na hatia ya makosa ya uhalifu wa kivita dhidi ya binadamu, na kuhukumiwa kifo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mahakama maalum, imempata na hatia hiyo, baada ya kubainika kuwa, alitoa maagizo kwa maafisa wa usalama kutumia nguvu dhidi ya maandamano yaliyoongozwa na wanafunzi mwaka uliopita.

Maafisa wa usalama, kwa kiasi kikubwa walitumia nguvu kupita kiasi kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa, ambapo watu zaidi ya 1,400 waliuawa kwa kupigwa risasi.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa ilisema kuwa polisi walitumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji.
Ripoti ya Umoja wa Mataifa ilisema kuwa polisi walitumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji. REUTERS – ABDUL GONI

Baada ya kupewa adhabu hiyo, Hasina, amesema, uamuzi wa Mahakama unaegemea upande mmoja na umechochewa kisiasa na wapinzani wake.

Hukumu yake, imetolewa baada ya kukimbilia nchini India, baada ya kuondolewa madarakani kufuatia maandamano.

Uamuzi huu, unatarajiwa kuiweka India kwenye shinikizo za kutaka Waziri Mkuu huyo wa zamani, kurejeshwa nchini Bangladesh, lakini wachambuzi wa siasa wanasema, hilo huenda lisifanyike.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *