Watu wenye silaha, wamewateka watu 25 katika shule ya sekondari ya wasichana, Kaskazini Magharibi mwa Nigeria.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Polisi wamethibitisha tukio hili, ambapo wamesema, watu hao walivamia shule hiyo na kuanza kufyatua risasi, kuanzia saa 10 Alfajiri katika jimbo la Kebbi.

Wakati polisi walipowasili katika shule hiyo ya serikali, ripoti zinasema, watu hao wenye silaha walikuwa wametoroka.

Miongoni mwa watu waliotekwa ni wanafunzi 25 ambao waliondolewa kwa nguvu kutoka kwenye mabweni yao na kupelekwa kusikojulikana.

Ripoti zaidi zinasema Naibu Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, ameuawa baada ya kupigwa risasi huku mwalimu mwingine akijeruhiwa.

Hii sio mara ya kwanza, kwa Nigeria kushuhudia matukio ya utekaji. Mwaka 2014 magaidi wa Boko Haram, waliwateka wasichana wa Shule ya sekondari ya Chibok zaidi ya 200.

Eneo la Kaskazini mwa Nigeria, tangu mwaka 2009, limeendelea kukumbwa na utovu wa usalama, licha ya jitihada za serikali mbalimbali kuahidi kumaliza makundi ya kigaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *