Kikao hicho kimeongozwa na Rais wa Sierra Leone, Julius Maada Bio, na kimejumuisha hotuba kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, na Rais wa Tume ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (CEDEAO), Omar Alieu Touray.

Guterres: Hali ya usalama Afrika Magharibi na Sahel yatia wasiwasi

Katibu Mkuu António Guterres ameonya kuwa hali ya usalama Afrika Magharibi na eneo la Sahel inazidi kuwa ya kutisha, akitaja matukio ya hivi karibuni nchini Mali kama mfano wa kuongezeka kwa hali ya hatari katika eneo hilo.

Guterres ametaka nchi wanachama kuchukua hatua za haraka katika maeneo matatu:

  • Kuandaa mkakati mpya wa usalama, akisisitiza kuwa mgogoro wa kikanda unahitaji hatua za kikanda;
  • Kukabiliana na mzizi unaoendeleza ugaidi, ikiwemo changamoto za kijamii na kiuchumi;
  • Kudumisha ufadhili thabiti wa kibinadamu ili kukidhi mahitaji ya dharura katika maeneo yaliyoathirika.

Amesisitiza haja ya mshikamano wa kimataifa na wananchi wa eneo hilo wanaopitia “kiwango kisichokubalika cha mateso,” na akathibitisha kwamba Umoja wa Mataifa umejizatiti kushirikiana na serikali za eneo hilo kupitia Mwakilishi Maalum kwa Afrika Magharibi na Sahel.

Omar Alieu Touray, Rais wa Kamisheni ya ECOWAS, akihutubia mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu uimarishaji wa Amani Afrika Magharibi.

UN Photo/Eskinder Debebe

Omar Alieu Touray, Rais wa Kamisheni ya ECOWAS, akihutubia mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu uimarishaji wa Amani Afrika Magharibi.

CEDEAO: Ugaidi sasa ni tishio kwa eneo zima

Rais wa Tume ya CEDEAO, Omar Alieu Touray, ametoa onyo kali akisema kuwa ugaidi ambao hapo awali ulikuwa umedhibitika zaidi katika Sahel na Bonde la Ziwa Chad sasa umegeuka kuwa “Uwepo wa tishio kwa Afrika Magharibi yote, likiathiri nchi za Sahel na vilevile mataifa ya pwani.”

Matukio 450 ya ugaidi, vifo karibu 2,000 mwaka 2025

Kwa mujibu wa takwimu za Mtandao wa Tahadhari ya Mapema na Hatua wa CEDEAO, matukio 450 ya kigaidi yalirekodiwa kati ya Januari na Novemba 2025, yakisababisha vifo vya watu zaidi ya 1,900.
Ingawa Sahel ya kati inachukua karibu asilimia 80 ya mashambulizi na asilimia 85 ya wahanga, Touray amesisitiza kuwa “hakuna eneo ndani ya kanda hiyo lililo salama.”

Makundi ya kigaidi yaanzisha vita vya kiuchumi

Mbali na kuwaua raia wasio na hatia, Touray ameonya kuwa makundi ya kigaidi sasa yamefungua uwanja mpya wa mashambulizi, vita vya kiuchumi.

Makundi haya amesema yanazuia usambazaji na ugawaji wa bidhaa muhimu, hususan mafuta hatua zinazovuruga biashara ya kikanda, kupunguza shughuli za kiuchumi, na kuongeza mateso kwa mamilioni ya watu.

Rais wa Sierra Leone: vita dhidi ya ugaidi na ukatili viratibiwe

“Kama hatutachukua hatua kwa uthabiti, Sahel inaweza kuwa hifadhi ya kudumu kwa makundi ya kiislamu yenye misimamo mikali, katika umbali wa saa chache tu kutoka miji mikubwa ya dunia” amesema Rais wa Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio katika kikao hicho cha Baraza la Usalama.

Mwanajeshi wa Niger akilinda eneo la kimkakati huko Ouallam, Niger.

UN News/Daniel Dickinson

Mwanajeshi wa Niger akilinda eneo la kimkakati huko Ouallam, Niger.

Bio ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS ameongeza kuwa “Imefika wakati wa kuchukua hatua kwa ujasiri na kwa ushirikiano.”

Ameelezea hili kama “mfumo wa kuratibu unaolenga kuoanisha masuala ya usalama, utawala bora, na hatua za kibinadamu.”

Kuhusu usalama wa kanda, Rais huyo amebainisha kuwa mfumo wa Muungano wa Nchi za Sahel unaweza kuunga mkono ule wa ECOWAS na Muungano wa Afrika AU, huku Umoja wa Mataifa, kupitia Ofisi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika Magharibi na Sahel UNOWAS na Ofisi ya Kupambana na Ugaidi, ikisaidia kuratibu.

ECOWAS kuendelea kufungua mlango

Katika muktadha huu, amebainisha kuwa ECOWAS itaendelea “kufungua milango yake kwa Burkina Faso, Mali, na Niger hadi pale utakapowezekana kuunganishwa kikamilifu. Mabadiliko ya kisiasa hayapaswi kamwe kuzuia ushirikiano katika masuala ya usalama yanayoshirikiwa,” amesisitiza.

Julius Maada Bio ameonya kwamba makundi ya kigaidi, yanayosaidiwa na mitandao ya uhalifu na silaha za kisasa, “mara nyingi yamebeba silaha zaidi ya nguvu za kitaifa na hutumia ufinyu wa mipaka.”

Amependekeza kushirikiana kwa taarifa za kijasusi, usafirishaji wa anga, usimamizi wa vifaa, na msaada wa ufuatiliaji.

Rais huyo wa Sierra Leone amependekeza mkataba kati ya ECOWAS-UN-AU kwa ajili ya amani na mnepo katika Sahel, kulingana na Azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa 2719 (2023), linalopendekeza msaada wa kimfumo na endelevu wa Umoja wa Mataifa kwa operesheni za kusaidia amani zinazofanywa na Muungano wa Afrika.

Dawa haramu zateketezwa mjini Niamey, Niger.

Dawa haramu zateketezwa mjini Niamey, Niger.

Wito wa ushirikiano wa kikanda na kimataifa

Guterres na Touray wamesema kuwa kukabiliana na vitisho vinavyozidi kuongezeka kunahitaji ushirikiano imara zaidi kati ya nchi za Afrika Magharibi pamoja na msaada endelevu kutoka kwa jumuiya ya kimataifa.

Ujumbe wao kwa Baraza la Usalama umekuwa wazi, bila hatua za haraka na za pamoja, mgogoro huu unaweza kuvurga usalama katika eneo zima.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *