Jina kamili la kiongozi wa taifa hilo ni Basirou Diomaye Diakhar Faye mzaliwa wa Ndiaganiao katika mji wa M’bour miaka 45 iliopita.

Ukiskia majina yanaumba maana yake ni hii kwa lugha ya Serer inayozungumzwa na baadhi ya watu wa Senegal na Gambia, jina ‘’Diomaye’’ maana yake ‘’Mheshimiwa’’ sasa limetimia au vipi?

Amekuwa rais wa nchi hiyo tangu mwaka April 2024. Yeye na Waziri Mkuu wake Ousmane Sonko walikutana wakiwa maafisa forodha.

Mwaka 2014 urafiki wao ukaimarika zaidi, Sonko alipounda chama cha kisiasa cha PASTEF.

Diomaye Faye alimsaidia sana Sonko katika uchaguzi wa urais wa 2019, lakini Sonko alimaliza wa tatu na asilimia 16 ya kura.

Kufa kufaana, mwaka 2021 Faye akawa Katibu Mkuu wa chama cha PASTEF baada ya Sonko kukamatwa.

Mwaka 2022 alijaribu kuunganisha upinzani na kufanikiwa kushinda viti 56 katika bunge la wajumbe 165. Alijaribu kutafuta umeya wa eneo la Ndianganao, lakini hakufanikiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *