
Dar es Salaam. Kibarua cha Kocha Marcio Maximo ndani ya KMC kinazidi kuwa shakani baada ya leo timu hiyo kupoteza mchezo wa nyumbani wa Ligi Kuu dhidi ya JKT Tanzania kwa bao 1-0.
Matokeo hayo yanaifanya KMC kuendelea kujichimbia mkiani, ikibaki na pointi zao tatu, ikipoteza mchezo wa sita mfululizo.
Licha ya kuonyesha mchezo mzuri KMC imeendelea kuonyesha udhaifu kwenye safi yake ya ushambuliaji ikishindwa kutumia nafasi ilizotengeneza.
Bao la kipindi cha pili la likifungwa kwa beki wa KMC Anuary Kilemile dakika ya 61 limetosha kuamua mchezo huo uliopigwa Uwanja wa KMC Complex.
JKT ingeweza kuongeza ushindi wao lakini ikakosa utulivu kutumia nafasi zilizotengenezwa na mshambuliaji Paul Peter na kiungo Hassan Dilunga.
Ushindi huo unaifanya JKT kupaa kutoka nafasi ya Saba mpaka ya pili ikifikisha pointi 10 sawa na vinara Yanga, ikicheza jumla ya michezo saba,ikiwashusha Simba kwa nafasi moja.
Kichapo cha leo kutoka kwa JKT Tanzania, kimeifanya KMC ipoteze mechi ya sita mfululizo ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.
Na mechi zote hizo ambazo imepoteza, KMC imekuwa chini ya Maximo.