“Jioni ya jana, mtoto wa kike aliripotiwa kuuawa huko Khan Younis kwa shambulio la anga, huku siku iliyotangulia, watoto saba waliuawa katika Jiji la Gaza na Kusini nwa jiji hilo,” amesema Ricardo Pires, msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF.

Kinachohitajika kujua

  • UNICEF inasema watoto 67 wameuawa wakati wa usitishaji mapigano.
  • Vifo vya Wapalestina 280 na majeruhi 672 vimeripotiwa tangu usitishaji mapigano kuanza.
  • Familia zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula licha ya shughuli za baadhi ya masoko.
  • Mfumo wa afya wa Gaza unashindwa, na kuacha watoto bila huduma za matibabu.
  • Takriban watoto 4,000 wanahitaji kuhamishwa haraka kwa matibabu.

Katika taarifa yake, Bwana. Pires amewaambia waandishi wa habari kuwa “Kuna upande mmoja tu wa mgogoro Gaza ulio na uwezo wa kufanya mashambulio ya anga.”

Tangu Oktoba 11, siku ya kwanza ya usitishaji mapigano kati ya jeshi la Israeli na wapiganaji wa Hamas, angalau watoto 67 wameuawa katika “matukio yanayohusiana na mgogoro,” amebainisha msemaji wa UNICEF.

Maelezo yake yamejitokeza wakati shirika lisilo la kiserikali lamadaktari waio na mipaka au  ya Doctors Without Borders likiripoti kuwa msichana wa miaka tisa anapatiwa matibabu kwa jeraha la uso baada ya risasi kutoka kwa Ndege zisizo na rubani au drones za quadcopter kuripotiwa Jumatano.

Uharibifu unaenea kote Gaza ambapo mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kutafuta jamii zilizo katika mazingira magumu zaidi ambazo mara nyingi zimekimbia makazi yao mara nyingi tangu vita vilipozuka kufuatia mashambulizi ya kigaidi yanayoongozwa na …

Uharibifu unaenea kote Gaza ambapo mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kutafuta jamii zilizo katika mazingira magumu zaidi ambazo mara nyingi zimekimbia makazi yao mara nyingi tangu vita vilipozuka kufuatia mashambulizi ya kigaidi yanayoongozwa na Hamas nchini Israel.

Mamia wameuawa na kujeruhiwa

Kulingana na UNICEF, angalau watoto 67 wameuawa katika “matukio yanayohusiana na mgogoro” tangu usitishaji mapigano baina ya Hamas-Israel kutangazwa Oktoba 10, kwa kiwango cha watoto wawili kila siku.

Mfanyakazi wa muda mrefu wa misaada wa Umoja wa Mataifa, Dk. Rik Peeperkorn kutoka Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Ulimwenguni WHO, amesisitiza wasiwasi huo, akiongeza kuwa “ingawa kuna mapumziko ya vita, watu bado wanauawa.”

Takwimu za hivi karibuni kutoka Wizara ya Afya ya Gaza zinaonesha kuwa Wagaza 280 wameuawa na 672 kujeruhiwa tangu usitishaji mapigano uanze kutekelezwa, pamoja na miili 571 iliyopatikana kutoka kwenye vifusi vya maporomoko ya majengo.

Pamoja na hali ya usalama inayodorora, timu za misaada za Umoja wa Mataifa ikiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP zinaendelea kusukuma kupata fursa ya ufikiaji Mkubwa wa mkubwa wa watu Gaza wakiwemo mamia ya maelfu ya familia zilizohama na ambazo sasa ziko hatarini.

Mabasi yatumika kuingiza msaada

Shirika hilo sasa linatumia takriban mabasi 100 kila siku kuingiza Gaza yakiwa na mizigo ya msaada, kiasi cha karibu theluthi mbili ya lengo lake la kila siku “Hii ni hatua sahihi” amesema Abeer Etefa, Msemaji Mkuu wa WFP kwa Mashariki ya Kati, Afrika Kaskazini na Ulaya Mashariki.

Amebainisha kuwa ingawa usambazaji kutoka sekta ya biashara pia unaingia Gaza, tatizo kuu kwa wahusika wa Umoja wa Mataifa na wasio wa Umoja wa Mataifa “ni kwamba chakula hiki kinabaki kwenye vituo vya mipaka kwa siku nyingi na hivyo uwezekano wa kuharibika ni mkubwa.”

Kutoka ndani ya Gaza, Kiongozi wa Mawasiliano wa WFP eneo la Palestina, Martin Penner, ameelezea hali mbaya inayokabili watu wa eneo hilo waliochoka, baada ya zaidi ya miaka miwili ya vita.

“Mwanamke mmoja ametuambia kwamba anahisi mwili wake mzima unalia kwa aina tofauti za chakula, tofauti na chakula cha makopo na virutubisho vikavu ambavyo watu wamekuwa wakila kwa miaka miwili,” amesema.

Bei hazishikiki

Masoko yanarudi Gaza yakiwa na chakula, “lakini bei bado hazishikiki kwa wengi,” amesisitiza Bwana Penner akiongeza kuwa “Kuku mmoja unauzwa dola 25, kilo ya nyama dola 20. Watu wengi bado wanategemea msaada wa chakula, vifurushi vya chakula, na mkate kutoka kwenye maduka ya kuoka mikate.”

Mama  mmoja alimuambia kuwa hakumpeleka watoto wake sokoni “ili wasione chakula chote kilichopo ikiwa wataenda karibu na soko, anawaambia wafunge macho.”

Mwanamke mwingine katika mji huo amesema ananunua tofaa moja na kuigawa kati ya watoto wake wanne.

Wakati huo huo, huduma za afya katika Ukanda wa Gaza bado zimeharibiwa na hazitoshi kutibu waathirika wa majeraha makubwa na wale wanaohitaji huduma maalumu.

“Madaktari wa Gaza wanatuambia kuhusu watoto wanajua jinsi ya kuokoa lakini hawawezi,” amesema Bwana. Pires wa UNICEF, akieleza kwa waandishi wa habari orodha ya watoto “wakiwa na majeraha mabaya ya moto, majeraha ya vipande vya risasi, jeraha la mgongo, jeraha la ubongo kutokana na mshtuko, watoto wenye saratani ambao wamepoteza miezi ya matibabu. Watoto wachanga wanaohitaji huduma za dharura. Watoto wanaohitaji upasuaji ambao hauwezi kufanywa ndani ya Gaza leo.”

Takriban watoto 4,000 bado wanangoja kuhamishwa, wakiwemo Omyma wa miaka miwili “ambaye moyo wake unashindwa kwa sababu ya tatizo la kuzaliwa ambalo madaktari wa Gaza hawawezi kutibu. Anahitaji upasuaji haraka kuokoa maisha yake,” amebainisha Bwana Pires.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *