Katika siku ya kwanza ya mkutano wa G20, viongozi wa mataifa hayo tajiri, wametaka kupatikana kwa mpango thabiti wa kuleta amani kwenye nchi zenye mizozo huko Ukraine, Sudan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na eneo linalokaliwa la Palestina.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika kauli ya pamoja, viongozi hao wamesema wakati umefika kwa kupatikana kwa suluhu ya kudumu, katika nchi hizo kwa kuheshimu kanuni za mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu amani.

Baaada ya kikao cha ufunguzi kumalizika, viongozi wa Uingereza, Ujerumani na Ufaransa, walikutana kujadili mapendekezo ya Marekani ili kuimarisha mapendekezo yanayolenga kumaliza vita kati ya Ukraine na Urusi.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akiwa na viongozi wengine katika mkutano wa G20 nchini Afrika Kuisni, Tarehe 22 Novemba 2025.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akiwa na viongozi wengine katika mkutano wa G20 nchini Afrika Kuisni, Tarehe 22 Novemba 2025. AP – Gianluigi Guercia

Katika hatua nyingine, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ameonya kuwa mataifa ya G20 yapo kwenye hatari kubwa, wakati huu yanapoendelea kupambana kupata suluhu kwenye nchi zenye mizozo duniani.

Macron ametoa changamoto kwa viongozi wenzake, ambao amesema wameendelea kushindwa kupata suluhu ya mizozo inayoendelea na kuwahimiza, kushughulikia changamoto hizo kwa pamoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *