
Mke wa Rais Recep Tayyip Erdoğan, Emine Erdoğan, amesema kuwa kuna uwezekano wa kutatua matatizo ya nyakati hizi kupitia njia shirikishi.
Emine Erdoğan alituma ujumbe kwa njia ya video, kwenye jukwaa la 6 la Mkutano wa Viongozi Wanawake, uliofanyika jijini Bujumbura nchini Burundi chini ya uenyeji wa Angeline Ndayishimiye, mke wa rais wa nchi hiyo, Evariste Ndayishimiye.
Akiutakia mkutano huo heri na fanaka, Emine Erdoğan alibainisha kuwa dunia ya sasa imetawaliwa na idadi kubwa ya vijana, na watoto wapatao bilioni 2, wenye umri wa kati ya miaka 10 hadi 19.
Akisisitizia jukumu lililo mbele kwa sasa, Emine Erdoğan alisema kuwa fursa mbalimbali zikiwemo zile za kielimu na mazingira salama ya kuishi, huakisi mustakabali wa maisha.
“Wakati baadhi ya watoto wakishuhudiwa kuminywa kwa fursa, wapo wengine wanaokosa kabisa hata haki zao za kimsingi,” alisema.
Akionesha hali ya matabaka kwa sasa ulimwenguni, Emine Erdoğan alisema:
“Kwa upande mmoja, maisha ya watoto ni ya kushtua. Uraibu mbalimbali kama vile mitandao ya kijamii na michezo ya video imeathiri makuzi yao. Kwa upande mwingine, zaidi ya watoto bilioni moja hawana fursa za intaneti kwa ajili ya kujipatia elimu. Wakati wengine hula milo yao yenye kuhusisha vyakula vili zindikwa na kukabiliwa na tabia ubwete, huku watoto milioni 181 wakikabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula. Licha ya familia kuwa taasisi muhimu ya makuzi ya mtoto, zaidi ya watoto milioni 140 wamegeuka kuwa wakiwa.”