Balozi mdogo ndiyo aliyekuwa amepewa jukumu hilo, akiwa ni cheo cha chini cha balozi au waziri. Kulingana na Makumbusho ya Kitaifa ya Diplomasia Marekani, bado cheo hicho kinatumika kama mkuu wa ujumbe wa Marekani katika maeneo ambayo Marekani hayana uhusiano mzuri wa kidiplomasia na nchi hiyo.

“Balozi au mwakilishi wa ubalozi nchini Afrika Kusini anakuwepo pale tu kuthibitisha kuwa Marekani itakuwa mwenyeji wa mkutano wa G20; watapokea jukumu hilo mwishoni mwa hafla yenyewe, hawatokuwepo hapo kushiriki katika mazungumo rasmi,” Msemaji wa Ikulu ya White House Karoline Leavitt aliwaambia waandishi wa habari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *