
Kamanda mwandamizi wa jeshi la Sudan amewataka raia kuitikia wito wa Mkuu wa Majeshi Abdel Fattah al-Burhan kuungana na wenzao nchi nzima dhidi ya wapiganaji wa RSF.
Ali Hassan Bello, kamanda wa eneo la Kiulinzi la Blue Nile, aliwapongeza wanajeshi, vikosi washirika, na umma “kwa ushindi waliopata enep la Kordofan dhidi ya wapiganaji.”
“Ushidni tutaupata katika miji iliyobaki,” alisema katika taarifa iliyosomwa na shirika la habari la serikali SUNA.
Aliwaomba vijana wa Sudan kuitikia wito wa Mkuu wa Majeshi wa kutaka wajitolee dhidi ya wapiganji hao.
Wito wa nchi nzima
Siku ya Jumamosi, Burhan, ambaye ni mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Sudan, alitoa wito kwa nchi nzima dhidi ya wapiganaji wa RSF.
Siku ya Jumanne, jeshi lilisema kuwa limepata mafanikio makubwa katika maeneo kadhaa Kordofan baada ya makabiliano na RSF.
Jeshi limesema “maeneo muhimu” yako salama, na kuapa kuendelea na mapigano dhidi ya RSF “hadi nchi itakapokuwa haina uasi na ajenda ya mataifa ya kigeni.”
Wakati huohuo, Jeshi la Sudan limedungua ndege isiyokuwa na rubani siku ya Jumatano katika eneo la Al Obeid, mji mkuu wa Jimbo la Kordofan Kaskazini, walioshuhudia walisema.